Waziri Mkuu wa zamani wa Libya, Mahmoud Jibril amefariki Dunia jijini Cairo alipokuwa amelazwa baada ya kugundulika kuwa na Virusi vya Corona.

Mahmoud Jibril, ancien PM libyen, décédé des suites du Covid-19 ...

Jibril mwenye umri wa miaka 68 aliwahi kuwa kiongozi wa waasi waliomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo  Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011.

Kiongozi huyo wa zamani wa Libya amefariki hapo jana siku ya Jumapili hospitali jijini Cairo alipokuwa amelazwa kwa wiki mbili, amesema Khaled al-Mrimi, ambaye ni Katibu wa chama cha National Forces Alliance, kilichoundwa na Jibril mwaka 2012.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Aljazeera, Alilazwa Ganzouri Specialized Hospital jijini Cairo Machi 21 baada ya kupata mshituko wa moyo, na siku tatu baadaye akakutwa na Virusi vya Corona.

Enzi za uhai wake aliwahi kuwa mshauri wa maswala ya kiuchumi katika serikali ya Gaddafi kabla ya kujiunga na mapinduzi mwaka 2011.

The post Jibril afariki Dunia kwa Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.