Watu waliokufa kutokana na virusi vya corona nchini Marekani wamefikia 45,000 leo ikiwa ni idadi iliyopanda maradufu katika kipindi cha wiki moja, huku rekodi ya vifo vya kila siku nayo ikiongezeka kwa kiwango cha kutia wasiwasi. 

Hapo jana Jumanne Marekani ilirikodi vifo 2,750 kwa siku licha ya takwimu mpya kuonesha maambukizi ya kila siku yanapungua nchini humo.

Majimbo ya New Jersey, Pennsylvania na Michigan kila moja liliripoti vifo vya zaidi ya watu 800 kwa siku, huku jimbo la New York lililo kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona nchini Marekani lilirikodi vifo vya watu 481.

Marekani ndiyo taifa lenye visa vingi vya maambukizi ya virusi vya corona vinavyofikia 810,000 ambavyo ni karibu mara nne ya maambukizi nchini Uhispania, taifa la pili kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa corona duniani.

Chanzo Reuters, DW

The post Idadi ya watu wanaokufa kutokana na virusi vya corona yatia wasiwasi Marekani appeared first on Bongo5.com.