Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Idadi ya waliofariki duniani  kutokana na janga la  virusi  vya corona imepanda na  kupindukia watu 200,000 leo Jumapili,(26.04.2020)

Wakati  huo huo shirika la  afya ulimwenguni WHO likionya dhidi ya “kuwapo kwa dhana ya uimara ya mwili” kwa wagonjwa wanaopona, kunakoonekana  kuwa ni chombo cha mataifa  kujitayarisha  kufungua uchumi wao.

WHO inapinga, “hati”  hizo kwasababu  kupona  kutokana  na maambukizi  ya  virusi vya corona  huenda  kusimlinde mtu  kutopata maambukizi tena.

“Kwa sasa  hakuna  ushahidi  kwamba  watu  ambao  wamepona kutokana  na  maambukizi  ya  COVID-19 na  wana chembe cha kingamwili  wana uwezo  wa  kulinda  dhidi  ya  kupata  maambukizi mengine,” shirika  hilo  la afya la  umoja wa  Mataifa limesema  katika taarifa.

Wakati  huo  huo  mamia ya  mamilioni  ya  Waislamu  duniani  kote hawakuingia  katika misikiti  katika  siku  ya  pili  ya  mwezi mtukufu wa  Ramadhani na  kuepuka  kula  pamoja  kwa  makundi  katika familia  wakati  wa iftar kwasababu  ya  sera za kutokaa pamoja  na kuweka  umbali kati  ya  mtu  na  mtu.

The post Idadi ya vifo vya COVID – 19 yafikia 200, 000 Duniani, WHO yaonya juu ya dhana hii appeared first on Bongo5.com.