Hospitali ya Taifa Muhimbili, imefunga mashine tatu za kusafisha damu   katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana zenye thamani ya Shilingi Milioni 210.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 26, 2020 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha na kuongeza kuwa, Hospitali hiyo pia inatarajia kufunga mashine moja ya kumsaidia mgonjwa kupumua kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa waliopata maambukizi hayo.

"Tayari wagonjwa wanaohitaji kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa , pia Hospitali imefunga mtambo wa kuchuja maji wenye thamani ya Shilingi Milioni 28, na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi za kusafisha damu uliogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 12" imeeleza taarifa hiyo.