Maelfu ya watu nchini Uhispania leo hii wameruhusiwa kurejea kazini, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya corona, ambapo serikali iliweka marufuku ya kufanyika shughuli za kawaida.
Jumatatu ya Pasaka kwa taifa hilo haikuwa siku ya kitaifa ya mapunziko kwa raia badala yake waliruhusiwa kuondoka majumbani mwao, ikiwa hatua ya taratibu ya kuindoa marufuku iliyodumu tangu mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa makadirio ya vyombo vya habari, takribani 300,000 walirejea makazini mjini Madrid. Kabla ya hatua hiyo, watu ambao ajira zao zilionekana kuwa na ulazima kufanyika waliruhusiwa kufanya kazi.
Hata hivyo rekodi mpya ya maambukizi zinaonesha watu 3,477 wameambukizwa. Hayo ni katika kipindi cha masaa 24 yaliopita. Kwa kuizingatia idadi hiyo, jumla ya maambukizi nchini humo kwa sasa inafikia watu 169,496, ikionesha uelekeo wa kupatikana unafuu kwa taifa hilo lilishambuliwa vikali na virusi. Katika kipindi kigumu nchini Uhispania kulirekodiwa hadi maambukizi 8,000 kwa siku. Vifo vipya kwa leo ni 517 na kufanya jumla yake kuwa 17,489.
The post Hispania: Maelfu ya watu warejea kazini, ni mara ya kwanza tangu kuibuka kwa Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.