Kuna ushahidi wa wazi kwamba dawa moja inaweza kuwasaidia wagonjwa wa Corona kupona kutoka kwa virusi hivyo, kulingana na maafisa wa Marekani.

Dawa ya remdesivir inapunguza muda wa dalili kutoka siku 15 adi siku 11 kulingana na majaribio yaliofanywa katika hospitali katika maeneo mbalimbali duniani.

Maelezo kamili hayajachapishwa , lakini wataalam wanasema kwamba yatakuwa matokeo bora iwapo yatathibitishwa ijapokuwa sio suluhu ya moja kwa moja ya ugonjwa huo.

Dawa hiyo ina uwezo wa kuokoa maisha , kuondoa shinikizo katika hospitali na kusaidia baadhi ya masharti ya kutotoka nje kuondolewa.

Remdesivir mara ya kwanza ilitengenezwa kutibu ugonjwa wa ebola . Ni dawa ya kukabiliana na virusi na inafanya kazi kwa kushambulia enzymes ambazo virusi vinahitaji ili kuweza kuzaana ndani ya seli ya mwili wa mwanadamu.

 

Majaribio hayo yalisimamiwa na taasisi ya Marekani kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi NIAID.

Na watu wapatao 1.063 walishiriki. Baadhi ya wagonjwa walipatiwa dawa hiyo huku wengine wakipata tiba inayofanana na hiyo.

Dkt Anthony Fauci ambaye anaongoza shirika la NIAID alisema: Data inaonyesha kwamba Remdesivir ina nguyvu za wazi kwamba inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka.

Amesema kwamba matokeo hayo yanathibitisha , kwamba dawa hiyo inaweza kuzuia virusi hivyo, na kusema kwamba sasa wana uwezo wa kutibu wagonjwa.

Kiwango cha vifo kilikuwa asilimia nane kwa watu waliopatiwa Remdesvir na asilimia 11 kwa wale waliopatiwa tiba kama hiyo, lakini matokeo haya hayakuwa na umuhimu mkubwa , ikimaanisha kwamba wanasayansi hawawezi kubaini iwapo tofauti hiyo ni ya kweli.

Haijulikani ni nani anayefaidika . Je inawasaidia watu ambao wangepona kupona kwa haraka? ama inawasaidia watu kutopelekwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi kwa uangalizi zaidi?

Je dawa hiyo ilifanya vyema miongoni mwa vijana ama watu wazima? ama wale wasio ama walio na magonjwa mengine? Je wagonjwa wanahitaji kutibiwa mapema wakati virusi hivyo vinapoanza kuenea mwilini?

Haya yatakuwa maswali muhimu wakati maelezo kamili yatachapishwa , kwa kuwa dawa hiyo inaweza kuwa na faida mara mbili zaidi ya kuokoa maisha na kuweza kuondoa amri ya kutotoka nje.

Profesa parmar, ambaye ndie mkurugenzi wa majaribio ya MRC Clinical Trials Unit UCL , ambaye amesimamia majaribio hayo barani Ulaya alisema: Kabla ya dawa hii kutengenezwa na kusambazwa kila mahali duniani, vitu kadhaa vinahitaji kufanyika: Data na matokeo yanahitaji kuchunguzwa na wadhibiti ili kuona iwapo dawa hiyo inaweza kupewa leseni na baadaye wanahitaji mamlaka za mataifa husika kutoa maoni yao.

Huku haya yakifanyika tutatafuta data zaidi kutoka kwa majaribio hayo, na nyengine kuhusu iwapo dawa hiyo inazuia vifo vya Covid-19.

”Iwapo dawa hiyo itawazuia watu wanaohitaji , basi hatari ya hospitali kuzidiwa ni ndogo, na hiyo itamaanisha kwamba mahitaji ya watu kutokaribiana hayatahitajika”.

Profesa Horby , kutoka Chuo kikuu cha OXford , anaendesha majaribio makubwa ya dawa ya Covid-19.

Alisema: Tunahitaji kuona matokeo, lakini iwapo yatathibitishwa hayo yatakuwa matokeo mazuri na habari njema katika vita dhidi ya Covid -19. hatua zinazofuata ni kupata data kamili na kuweza kutoa usawa wa kupatikana kwa dawa ya remdesivir.

Data ya Marekani kuhusu remdesvir imetoka wakati mmoja na matokeo ya dawa kama hiyo nchini China, imeripotiwa katika jarida la lancent, kwamba haifai.

Hatahivyo, majaribio hayo hayakukamilika kwasababu ufanisi wa amri ya kutotoka nje mjini Wuhan kulimaanisha kwamba madaktari walikosa wagonjwa.

”Data hizi zinatoa matumaini , na kwasababu hatuna tiba ya moja kwa moja ya Covid, inaweza kufanya remdesvir kuidhinishwa kutibu Covid”, alisema Profesa Babak Javid, mshauri wa magonjwa ya maambukizi katika hospitali ya Cambridge.

Jinsi chanjo ya corona itakavyofanya kazi

Hatahivyo pia inaonyesha kwamba remdesvir sio suluhu wakati huu: faida ya kumsaidia mtu kupona ni asilimia 30. Dawa nyengine zinazochunguzwa kutibu Covid-19 ni pamoja na zile za malaria na HIV ambazo zinaweza kushambulia virusi hivyo pamoja na kuwa dawa zinazoweza kulinda kinga ya mwanadamu.

Lakini inaonekana kana kwamba dawa hizo za kukabiliana na virusi zinaweza kupewa mgonjwa mapema wakati anapoanza kuugua maradhi hayo na baadaye kupatiwa dawa za kulinda kinga katika awamu za mwisho mwisho za ugonjwa huo.

Chanzo BBC

The post Hii ndio dawa yenye nguvu za kukabiliana na makali ya virusi vya corona appeared first on Bongo5.com.