Bongo5TV imepita mitaa ya ofisi za Wasafi baada ya Diamond siku ya jana kutangaza kwamba anamtambulisha msanii mpya wa label hiyo. Katika mitandao ya kijamii kuna mengi yanazungumzwa kuhusu nani atatangazwa leo huku baadhi ya wadau wakidai ni Zuchi au Hanstone.
Wadau wa mambo wanadai lebo hiyo yenye wasanii wenye nguvu nchini Tanzania tayari ina wasanii sita benchi ambao wanasubiri muda wa kutangazwa. Bongo5TV ilikutana na Juma Lokole mmoja kati ya watangazaji wa Wasafi Fm na kuzungumza naye mambo kadhaa kuhusiana na msanii huyo mpya.
The post Hali ya ofisi za Wasafi kwenye harakati za kumtangaza msanii mpya, Juma Lokote aangukia kwa Hanstone na Zuchu (Video) appeared first on Bongo5.com.