Taarifa kubwa kwa leo ni hii inayomhusu Kiongozi wa Korea Kaskazini bwana Kim Jong Un ambayo inaripotiwa kuzidi kuwa mbaya zaidi.
Baada ya taarifa hizo imeelezwa kuwa taifa la China tayari limetuma timu ya Madaktari kwenda Korea Kaskazini kwa lengo la kutoa ushauri kuhusu afya ya Kim Jong Un, ripoti kutoka China zinasema timu hiyo imefikia uamuzi huo kufuatia ripoti za kuugua kwa Kim ingawa Korea Kaskazini bado haijathibitisha kama kweli Kiongozi wake huyo anaumwa.
Mbali na taarifa hizo kutoka China pia Rais wa Marekani bwana Donald Trump amezungumzia hali ya kiafya ya kiongozi huyo ambaye amedai ni rafiki yake na amesema ana amini Kim Jong Un ni mzima kabisa na taarifa kuhusu kuugua kwake ni za uzushi tu, lakini Trump amekataa kusema iwapo amewasiliana na Kim au Maafisa wa Korea Kaskazini siku za karibuni au laah.
•
“Nina mawasiliano mazuri sana na Kim Jong Un na naamini yuko salama, nadhani zile ni taarifa za uzushi tu zilizoanza kupikwa na CNN kuwa Kim anaumwa”
The post Hali ya kiafya ya kiongozi wa Korea kaskazini yaelezwa kuwa mbaya, China yatuma madaktari Trump atoa kauli hii – Video appeared first on Bongo5.com.