Kasi ya kuenea na madhara ya ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) hutofautiana sana baina ya watu. Japo asilimia 80 ya ambao wameambukizwa wamepata dalili za wastani kama vile dalili za kama mafua, kwa upande mwingine kuna wale walioishia kupata homa ya mapafu na kuwekwa kwenye mashine ya kuwasaidia kupumua kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo suala la kupona kabisa si mara zote ni jambo la kutumainiwa.
Hata hivyo, kila baada ya siku, vifo vipya hurekodiwa ikiwemo vya vijana wa kiume na wa kike na hata watoto ambao walikuwa na afya madhubuti kabla ya kukumbwa na corona.
Kwanini? Unawezaje kueleza kwa nini watu ambao hawako kwenye kundi la watu walio katika hatari zaidi huathirika sana au hata kufa kutokana na virusi vya Covid-19?
”Hilo ni swali muhimu sana,” Michael Snyder, Profesa na Mkurugenzi wa Idara ya jenetiki katika Chuo kikuu cha Stanford nchini Marekani, ameiambia BBC,kwasababu ni vigumu kupata jibu.
Lakini ingawa kutegua swali hili si kazi rahisi, wanasayansi wanahisi jibu linaweza kupatikana (kutokana na sababu za kijenetiki au kimazingira, wanasema), na wameanza kufuatilia tafiti mbalimbali ili kupata mwanga kuhusu swali hili.
Kuelewa ni kwa nini watu ambao ambao hawana maradhi hushambuliwa na ugonjwa huo, wanasema, itaruhusu wale walio hatarini zaidi kutambuliwa, matibabu mapya na madhubuti – pamoja na chanjo – kuundwa na na dawa zilizopo kutumika.
Nadharia ya jeni

Mojawapo ya nadharia ambazo zimependekezwa na ambazo zinaongezea uzito ni ile ya
Hii ni kwa msingi wa wazo kwamba sura zetu wenyewe za maumbile zinaweza kushawishi uhalifu ambao virusi huathiri mwili wetu.
Sio wazo jipya. Kutoka kwa tafiti kulinganisha mapacha na mapacha, tunajua kuwa uwezekano wa magonjwa makubwa ya kuambukiza ulimwenguni kama ugonjwa wa kifua kikuu, homa ya ini au ugonjwa wa Malaria, hutofautiana kwa sehemu kulingana na tabia ya maumbile,” Stephen Chapman anafafanua kwa BBC World, mtaalam wa magonjwa ya kupumua na mtafiti wa jeni ya Binadamu huko kituo cha wellcome katika Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza.
Mfano ambao wanasayansi kadhaa, pamoja na Chapman, hutumia kuelezea uzito wa jeni ni ile ya virusi vya herpesx.
Hivi ni virusi vinavyoenea kwa kiasi kikubwa kwa watu ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi kwa njia ya mdomo au uso, ikiwa ni aina moja, au vidonda kwenye sehemu ya siri, ikiwa ni aina nyingine.
“Idadi kubwa ya watu wanaopata maambukizi ya virusi huwa hawaugui sana.”
“Nadharia ni kwamba ikiwa una aina fulani, ambayo inaweza kufanya iwe rahisi au vigumu zaidi kwa virusi kuingia kwenye seli, kwa hivyo inaweza kukufanya uwe rahisi au vigumu zaidi kupatwa na ugonjwa huo,” anafafanua mtaalam huyo.
Kwa maoni ya Jean-Laurent Casanova, profesa na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Rockefeller huko New York, Marekani, tofauti hizi za jeni (au, kama anavyoita, kasoro za kuzaliwa), “inaweza kuwa katika hali ya utulivu mpka maambukizi yanapojitokezaya mwisho kwa miongo kadhaa, hadi maambukizi yanapotokea.
Kwa sababu hiyo maabara yake sasa inachunguza kama hali hii inatokea wakati huu wa maambukizi ya virusi vya corona.
Chapman anaamini kuwa mtu kuwa hatari ya kuambukizwa huenda si kuwa inategemea jeni za namna mbalimbali, bali jeni kadhaa, kujumuisha na sababu mbalimbali zinazojitokeza katika maisha.
Aina mbalimbali , anaeleza mtafiti huyu kuwa, zinaweza kuwa katika jeni zinazohusiana na mfumo wa kinga
Kromosomu X

Jambo lingine anasema mtafiti, ni ikiwa kuna jeni ndani ya kromosomu (nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni) X ambayo inachochea athari za ugonjwa huo, kwani wanaume wanaonekana kuathiriwa zaidi na ugonjwa mpya kuliko wanawake.
Maelezo ya utafiti mmoja uliofanyika China yanasema kuwa wanaume wako kwenye hatari kutokana na mtindo wa hatari wa maisha wanayoishi kutokana na tabia zinazohusishwa na tumbaku na vilevi.
Haijulikani kwanini hasa mfumo wa kinga hufanya kazi kwa baadhi ya watu kwa namna hii, lakini jibu kinaweza kuwa kwasababu ya Jeni.
”Tunafahamu kuwa kuna mabadiliko ya nadra katika jeni ambayo husimamia mfumo wa kinga,” anasema Chapman.
Kama mtaalam wa masuala ya kijenetiki, Michael Snyder kamwe haoneshi umuhimu wa jeni, lakini anaamini kwamba katika suala hili kuna sababu nyingine ambayo inaweza kuwa na uzito zaidi na hiyo ni mazingira: mawasiliano ya hapo awali na kirusi kingine cha corona.
Wingi wa virusi

Sababu nyingine ya athari kubwa kwa wagonjwa ni wingi wa virusi wakati wa maambukizi.
”Tunajua kutokana na tafiti nchini China kuwa wale wanaowahudumia wagonjwa walioathirika na virusi vya corona wako hatarini kuliko wengine kwasababu wako kwenye mazingira ya maambukizi kila siku wakati wanapokuwa kazini,” ameeleza mtaalamu stadi za sayansi ya virusi Alice Sinclair kutoka Chuo Kikuu cha Sussex, nchini Uingereza.
”Lakini hatujui kama ni kwa sababu ya wingi wa virusi ambavyo wanakumbana navyo kwenye shughuli zao au idadi ya watu wanaowahudumia.”
Hata hivyo jibu hili si hitimisho, miongoni mwa mambo mengine, kutokana na kile kilichogundulika hivi karibuni kuhusu wingi wa virusi vya corona, ni kama vile ukweli kuwa mtu mwenye dalili anaweza kuwa na idadi kubwa ya virusi.
Kwamba mtu anaweza kuwa na virusi vingi lakini asiwe mgonjwa sana au asioneshe dalili.
Ndio maana kuepuka kuchangamana ni moja kati ya hatua ambazo serikali na wataalamu wa afya wanasisitiza zaidi kuepuka kusambaa kwa virusi, anasema mtafiti.
Kuathirika na virusi vingine vya corona

”Inawezekana kuwa kuna kitu kinachosukuma mfumo wa kinga mwilini,” anasema Synder akizungumza na BBC.
Hisia zake anazielekeza kwa “virusi vingine vya corona ambavyo vinazunguka na ambavyo havijazungumzwa sana, vinavyoitwa HCoV-229E, na hivyo inaleta homa ya mafua.”
”Hatujui kama kuathirika na homa ya mafua (ambayo si hatari kama Covid-19) kunaweza kuimarisha zaidi kinga au, kukufanya kuwa na hatari ya kuambukizwa,” anasema mtaalamu.
”Lakini ninafikiri inaweza kuwa na athari kubwa,” anaongeza.
”Inawezekana kuwa watu wengi waliathirika katika miaka ya karibuni (na virusi hivyo vya corona) na hawajui, kwasababu waliona kama mafua ya kawaida.”
The post FAHAMU: Nadharia zaonyesha hata vijana wenye afya njema, Wana uwezekano mkubwa wa kufa kwa Corona appeared first on Bongo5.com.