Tarehe 12 Januari – chini ya miezi mitatu iliyopita- virusi vya coronavirus vilikua ndani ya Uchina pekee. Hapakua na kisa hata kimoja kilichokua kimepatikana nje ya nchi hiyo ambako virusi hivyo vilianzia.

Don't breathe on me! Kim Jong-un forces guards to wear masks amid ...

Halafu 13 Januari, virusi hivyo vikaanza kuwa tatizo la dunia. Kisa cha kwanza kilirekodiwa Thailand kabla ya Japan, Korea Kaskazini zikafuatia haraka.

Katika maeneo mbalimbali ya dunia visa vikaanza kuongezeka. Kwa sasa zaidi ya visa milioni moja vya Covid-19 kote duniani, kutoka katika nchi kama Nepal Nicaragua.

Lakini Je huku idadi ya vifo ikiongezeka, na hospitali zikifurika wagonjwa, bado kuna sehemu ambazo hazina kabisa virusi vya corona?

Jibu huenda linaloweza kukushangaza ni , ndio.Nchini Korea Kaskazini hakujakuwepo na visa vilivyoripotiwa pamoja na majaribio zaidi ya makombora

Nchini Korea Kaskazini hakujakuwepo na visa vilivyoripotiwa pamoja na majaribio zaidi ya makombora

Kuna nchi 193 ambazo ni wanachma wa Umoja wa Mataifa. Kufikia tarehe 2 Aprili, nchi 18 zilikua zimeripoti visa vya Covid-19 kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Nchi 18 zisizo na Covid-19

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC,  Visiwa vya Comoro; Kiribati; Lesotho; Marshall Islands; Micronesia; Nauru; Korea Kaskazini; Palau; Samoa; Sao Tome na Principe; Visiwa vya Solomon ; Sudan Kusini ; Tajikistan; Tonga; Turkmenistan; Tuvalu; Vanuatu, na Yemen

Baadhi ya wataalamu wanaafikiri kuwa nchi hizi zinaweza kuwa na visa ambavyo havijaripotiwa. Korea Kaskazini kwa mfano, rasmi haina kisa cha coronavirus sawa na Yemen inayokumbwa na vita.

Lakini kuna nchi ambazo virusi havijafika. Vingi kati ya visiwa vidogo vyenye wageni wachache – saba kati ya visiwa 10 ambavyo havitembelewi duniani kulingana na data za Umoja wa Mataifa ,viko huru na Covid-19.

Umbali wake na maeneo mengine – unamaanisha kuwa sheria ya kutosogeleana tayari ndiyo maisha wanayoishi.

Hata hivyo rais wa moja ya visiwa hivyo ameimambia BBC kuwa Covid-19 ni jambo la dharura kwao

Nauru, Kisiwa kilichopo katika bahari ya Pacific , kiko takriban maili 200 kutoka eneo lolote jingine – Kisiwa cha Banaba, sehemu ya Kiribati, ni kisiwa kilichopo karibu zaidi . Mji mkuu uliopo karibu ni Brisbane, uliopo maili 2,500 kusini -magharibi ambako inawabidi wasafiri kwa ndege kufika huko.

Kisiwa hiki kina takriban watu 10,000, ikiwa ni idadi ndogo zaidi baada ya ile ya wakazi wa Tulavu.

Ni moja ya maeneo ambayo yanatembelewa na watu wachache zaidi duniani. Ingawa hakionekani kwenye data nyingi za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa , mmoja wa watu wanaoendesha shughuli za utalii anasema nchi hiyo hupata watalii 160 tu kila mwaka.

Unaweza kudhani kuwa maeneo hayo ya mbali kiasi hicho haya hitaji kujitenga zaidi. Lakini nchi yenye hospitali moja , bila vifaa vya kuongezea wagonjwa hewa ya kupumua, ukosefu wa wauguzi haziwezi kuacha kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi.

  • Tarehe 2 Machi wasafiri walizuiwa kutoka Uchina, Korea Kaskazini, na Italia. Siku tano baadae Iran iliongezwa kwenye orodha hiyo
  • Katikati ya mwezi Machi, Nauru Airlines ilisitisha safari za ndege za kuelekea Fiji , Kiribati na Visiwa vya Marshall na kupunguza safari za kuelekea – Brisbane – kutoka hadi mara tatu kwa wiki hadi mara moja.
  • Baada ya hapo wale waliokua wanawasili kutoaka Australia waliamrishwa kujitenga katika karantini kwa siku 1 katika hoteli.

The post Fahamu Mataifa ambayo hayajaripoti maambukizi ya Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.