Katika nchi zinazopambana na virusi vya corona, madaktari na wauguzi wanasifiwa kwa ushujaa wao wakiwa mstari wa mbele katika kupambana na virusi vya corona.

Lakini pia janga hili limeonyesha unyanyapaa mkubwa kutoka kwa baadhi ya wagonjwa.

Daktari Roghieh Dehghan alizaliwa Iran, akasomea Austria na amekuwa akiishi na kufanyakazi London kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kama daktari na mtafiti.

Muda mfupi tu baada ya kuthibitishwa kupatikana kwa virusi hivyo Uingereza, alibaguliwa.

“Mwanamme mmoja mwenye umri mkubwa alikuja katika mgahawa wa eneo langu na akaanza mijadala ya kawaida tu kuhusu virusi vya corona, akawa anazungumza na kila mtu kwa sauti kubwa tu isipokuwa mimi,” anasema Daktari Dehghan.

Dr Roghieh Dehghan sitting at her deskHaki miliki ya pichaROGHIEH DEHGHAN
Image captionDaktari Roghieh Dehghan aliambiwa arejee kwao akiwa kwenye mgahawa mmoja, London

“Alisema kwamba maambukizi yote yanatokea nchi za nje, na kusambazwa na raia wa kigeni wanaoingia kwa boti. Aliniuliza ninatoka wapi. Sikusema lolote, Nilikuwa ninajitahidi nisimsikilize. Na akasema, ‘Oh, wewe ni raia wa kigeni hapa. Rudi kwenu.”

Wakati mhudumu wa mgahawa alipojaribu kumtetea daktari Dehghan, akielezea kwamba yeye kama daktari, alikuwa anasaidia nchi, mwanamume huyo aliendendelea kumkemea tena kwa ukali zaidi.

Tukio hilo lilimkasirisha sana na kumuacha akiwa amechanganyikiwa kuhusu nafasi yake katika jamii hiyo.

“Kwa sasa, nchi yangu inahitaji lakini kunihitaji na kunitaka ni vitu viwili tofauti kabisa. Ni kama uhusiano wenye mapenzi na chuki ndani yake,”anasema Daktari Dehghan.

” Siwezi kujitenga, Siwezi kwenda kazini na kusema, ‘Ukweli wa kwamba mimi ni mhamiaji nitauacha nyumbani na kuingia kazini nikiwa kama daktari tu.’

“Nahisi kabisa sithaminiwi sio tu na watu kama yule mwanaume aliyekuwa mgahawani, baadhi ya sehemu inaegemea mtu wa tabaka la juu huku sehemu nyengine ikionesha kwamba wewe umekataliwa. Kile ninachofanya kina maana kubwa kwangu, lakini vile nilivyo mimi si chochote si lolote.”

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba watu waliozaliwa nje ya Uingereza ni karibia robo nzima ya wafanyakazi wote wa afya nchini humo na daktari Dehghan anatumai kwamba mlipuko wa virusi vya corona utalazimisha watu kufahamu hilo.

“Sinahaja na kupigiwa makofi mitaani,” anasema. “Ninachotaka ni watu kutathmini tena uhusiano wao na wahudumu wa afya – sio tu kile tunachofanya lakini pia sisi ni kina nani.”

Nimekulia New York – Nishapitia ubaguzi

Dr Edward Chew wearing a visor and protective maskHaki miliki ya pichaEDWARD CHEW
Image captionDr Edward Chew anasema kuwa yeye pekee ndie aliyetakiwa kuonesha cheti chake cha kazi wakati ananunua bidhaa za kujikinga kwa ajili ya timu yake.

New York imejitokeza kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona Marekani na hadi sasa mji huo umethibitishwa kuwa na visa vingi zaidi.

Dr Edward Chew ndie anayesimamia idara ya dharura katika hospitali kubwa ya Manhattan na inajaribu kukabiliana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu walio katika hali mahututi tena kwa haraka mno.

Anasema kwamba baadhi ya watu wanazungumza nae kwa mitazamo tofauti, kwasababu ni raia wa Marekani mwenye asili ya Asia na pia kuna baadhi ya wagonjwa wanaoomba kuonekana na daktari mwengine.

“Nilikulia New York. Nimepitia ubaguzi,” anasema Daktari Chew. “Lakini hata siku za mwanzo za virusi hivyo, niligundua kwamba watu waliokuwa karibu na mimi walikuwa wakizungumza kwa kunong’ona huku wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini.”

Kukiwa na wasiwasi kwamba huenda kukawa na ukosefu wa vifaa vya kujilinda dhidi ya virusi vya corona, alienda kununua vifaa vya ziada kwa ajili ya timu yake.

“Niliona watu wakinizungumza wakati nikiwa nimeunga foleni nikisubiri kuhudumiwa. Mimi peke yangu ndio niliyehitajika kutoa vyeti vyangu ili kuthibitisha kwamba kweli mimi ni mhudumu wa afya kununua miwani na barakoa za usoni,” anasema.

“Katika duka moja, vijana watatu walinifuata na kuanza kukohoa bila adabu huku wakinikaribia. Nilipolipa na kuondoka, walinifuata hadi eneo la kuegesha gari na kuanza kunitendea vitendo vya kunibagua.”

Dr Edward Chew wearing his blue medical shirtHaki miliki ya pichaEDWARD CHEW
Image captionDr Edward Chew anasema kwamba ubaguzi aliopitia bado hakujabadilisha nia yake ya kusaidia jamii.

Daktari Chew anasema kwamba wakati wote amekuwa akichukulia New York kama mji wenye kukumbatia utamuduni mbalimbali.

Licha ya kile ambacho amepitia hivi karibuni, bado anasisitizia dhamira yake ya kusaidia hata wakati ambapo janga la corona linaendelea kuwa baya zaidi.

“Mgonjwa ni mgonjwa. Sijali wanavyonichukulia, au kile wanachonifikiria. Virusi hivi havibagui na tunapomuona mtu mwenye virusi hivi ni jukumu letu kumsaidia,” anasema.

“Najitahidi kuendelea kuwa na matumani, lakini ni wazi kwamba hiki ni kipindi kigumu zaidi ambacho sijawahi kukishuhudia katika taaluma yangu ya utabibu.

“Kufanyakazi katika idara ya dharura, nimewahi kufanyakazi katika mazingira ya shinikizo hapo kabla, lakini sijawahi kuwa kwenye hali ambapo kile ambacho unakabiliana nacho kinaweza kuua tena kwa haraka sana.”

Daktari anaweza kuwa wa muhimu zaidi

Australia Gold Coast, daktari wa upasuaji Rhea Liang anasema kwamba atakuwa mwenye bahati ikiwa atapata muda wa kulala hata kama ni kidogo tu, kwasababu ya janga la corona.

Huku idadi ya waliothibitishwa uambukizwa virusi hivyo ikisemekana kuwa ya chini, daktari Dr Liang anasema watu wamemhusisha na usambaaji wa virusi vya corona.

“Bado huwa napata maoni watu wanaponiona, na kusema, ‘Oh lakini China ndio chanzo cha ugonjwa huu kwa kula wanyama wa porini.”

Dr Rhea Liang smiling in an operating theatreHaki miliki ya pichaRHEA LIANG
Image caption“Jukumu langu la msingi ni kuhakikisa natoa huduma bora za afya bila kuhukumu yeyote,” anasema daktari Rhea Liang

Wakati wa kushauriana na mgonjwa, daktari Liang anasema mgonjwa mmoja alikataa kumtambua “na kutania” kwamba yeye ni raia kutoka China,” anasema.

“Niliendelea tu na ushauri wangu. Unajua falsafa yangu? Mtibu mgonjwa kwanza,” anasema.

Daktari anaweza kuwa na umuhimu mkubwa. Unaweza ukashindwa kujua hasa mgonjwa anatatizo gani kwasababu anahofu au ana msongo wa mawazo.

“I wish no one was racist and it’s clearly something we will have to work harder to counter when this is over, but for now I try to take the mantra that none of us is an angel, and my primary obligation is to provide the best medical care without judging people.”

Dr Liang is heartened that most people are supporting her and her team, now that the scale of the global challenge has become a stark reality.

“Funnily enough, the racism seems to have subsided a bit as the pandemic progresses and it becomes clear that we’re all in this together,” she says.

“On the frontline, there is such diversity and all of us are pulling together to get the job done.”

The post Fahamu jinsi Madaktari wanavyokumbana na ubaguzi wakitibu wagonjwa wa Covid-19 appeared first on Bongo5.com.