Winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, hana mpango wa kujiunga na Chelsea, hatua ambayo inaiweka Manchester United katika nafasi nzuri ya kupata saini yake japo Real Madrid pia wanapigiwa upatu kumsajili nyota huyo. (Diario Madridista, in Spanish)

Jadon Sancho

Barcelona wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham mfaransa Tanguy Ndombele, 23. (Star)

Everton wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez. Manchester United na Juventuspia wanamnyatia nyota huyo wa miaka 28. (Express)

Everton wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez.Everton wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez.

Chelsea inatarajiwa kuwasilisha ofa ya pili ya kumnunua mchezaji mahiri wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens. Klabu hiyo iliwasilisha ofa ya kwanza ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 32- Januari na kukataliwa, lakini Mertens hajatia saini mkataba mpya na klabu yake ya Italia. (Gazetto dello Sport, in Italian)

Roma haijakubali kufikia bei ya Arsenal ya £22m kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan. Muarmenia huyo wa miaka 31, yupo klabu hiyo ya Italia inayoshiriki Ligi ya Serie A kwa mkopo wa msimu mzima. (Calciomercato, via Star)Roma haijakubali kufikia bei ya Arsenal ya £22m kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh MkhitaryanRoma haijakubali kufikia bei ya Arsenal ya £22m kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan

Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez, 22, huenda akajiunga mchezaji mwenza wa Argentina Lionel Messi katika klabu ya Barcelona, amesema ajenti wake. Manchester City ilikuwa imatarajiwa kumsaini hakiungo huyo wa miaka 22. (Fox Sports Mexico, in Spanish)

Hatahivyo, naibu rais wa Inter Milan Javier Zanetti anaamini Martinez atasalia katika klabu hiyo. (ESPN)

Beki wa Inter Milan na Uruguay Diego Godin huenda akahamia Ligi ya Premia msimu huu wa joto. Manchester United na Tottenham pia wanamtaka mchezaji huyo wa miaka 34. (Tuttosport, in Italian)Beki wa Inter Milan na Uruguay Diego Godin huenda akahamia Ligi ya PremiaBeki wa Inter Milan na Uruguay Diego Godin huenda akahamia Ligi ya Premia

Mwenyekiti Tottenham Daniel Levy huenda akapinga uhamisho wa mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Willian, anasema beki wa zamani wa England Danny Mills. Mchezaji huyo wa miaka 31-aliwahi kupuuzilia mbali uhamisho wa kuenda Spurs mwaka 2013 baada ya kupita vipimo vya kimatibabua. (Football Insider)

Mkufunzi wa Southampton Ralph Hasenhuttl amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa miaka mitatu. (Sun)Mwenyekiti Tottenham Daniel Levy huenda akapinga uhamisho wa mshambuliaji wa Chelsea na Brazil WillianMwenyekiti Tottenham Daniel Levy huenda akapinga uhamisho wa mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Willian

Arsenal wanajaribu kubana matumizi ya karibu £25m kwa kuwapunguzia marupu rupu wachezaji ikiwa hawatafuzu kwa Champions League. (Telegraph, subscription required)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice amesema angelipendelea kucheza tena na mwezake wa Chelsea Mason Mount. Wawili hao, ambao wote wana miaka 21, walikuwa pamoja katika chuo cha mafunzo ya soka cha Chelsea. (Copa90)Phil Jones

Winga muingereza Phil Jones, 28,amesema kuwa aliukataa ombi la kujiunga na Manchester City, Liverpool na Arsenal kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2011. (MUTV)

The post Everton, United na Juventus vitani kuwania saini ya mshambuliaji huyu wa Real Madrid, wengine sokoni appeared first on Bongo5.com.