Wawakilishi wa Mataifa 19 ya ukanda wa sarafu ya Euro wamekubaliana kutolewa mara moja kiasi cha Euro bilioni 500 kwa ajili ya kuuimarisha uchumi wa Ulaya.
Hatua hiyo imefikiwa wakati ikipambana kunusuru kuanguka kwa uchumi kutokana na janga la corona.
Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno La Maire amesema makubaliano hayo ni mazuri mno. Mataifa makubwa kiuchumi Ulaya, ya Ujerumani na Ufaransa yamekuwa yakipambana kupata suluhu ya kushughulikia athari za kiuchumi kufuatia janga hilo, wakati mawaziri wa fedha wakijadiliana kuhusu suala hilo jana Alhamisi.
Waziri wa fedha wa Ujerumani, Olaf Scholz amesifu uamuzi huo akitaja kama siku njema kwa mshikamano wa Ulaya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliomba baraza la usalama la Umoja huo kuonyesha mshikamano, wakati lilipokutana na kujadiliana kuhusu janga la virusi vya corona. Guterres amesema mbele ya baraza hilo lililogawanyika kwamba ishara ya mshikamano ya wanachama wake 15 itasaidia pakubwa katika wakati huu wa mashaka.
Kikao hicho cha kwanza cha baraza hilo kimefanyika kwa siri kupitia video, lakini Umoja wa Mataifa ulichapisha hotuba ya katibu mkuu. Baraza hilo linakutana baada ya wiki kadhaa za kutokukubaliana, hususan kati ya Marekani na China, ambako janga hilo lilianzia mwezi Disemba mwaka jana.
The post Euro Bilioni 500 kutumika kunusuru uchumi wa Ulaya appeared first on Bongo5.com.