Mamlaka ya dawa ya Umoja wa Ulaya imeonya kuwa dawa za malaria zinazotumiwa kwa majaribio kutibu ugonjwa wa covid-19, zinaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwemo kifafa na matatizo ya moyo.

Mamlaka hiyo imesema katika taarifa kuwa dawa za Chloroquine na hydrxychloroquine – zinazopigiwa upatu na rais wa Marekani Donald Trump na wengine kama zinazoweka kuwa tiba mujarabu ya covid-19 – zinajulikana kusababisha matatizo ya mapigo ya moyo, hasa inapochanganywa na dawa nyingine.

Mpaka sasa hakuna tiba iliyoidhinishwa kwa ajili ya covid-19 na majaribio kadhaa yanaendelea kote duniani. Dawa za chloroquine na hydroxychloroquine zimetumiwa kwa muda mrefu kutibu malaria, na magonjwa ya maumivu.

Mbali na uwezekano wa kusababisha matatizo ya moyo, dawa hizo mbili zinaweza pia kuwa na madhara mengine yakiwemo kuharibu ini na figo, na pia kusababisha kushuka kwa sukari mwilini.

Chanzo DW

The post EU yaonya dawa za Malaria zinazotumiwa kwa majaribio dhidi ya COVID – 19 appeared first on Bongo5.com.