Borussia Dortmund itamuongezea mshahara wa paundi milioni 3.5 winga wa Uingereza Jadon Sancho, 20, ikiwa atakataa ombi la kuhamia Premier League (Bild, via Mirror)

Sancho

Newcastle huenda ikaonesha wazi nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Chile na mchezaji wa Barcelona Arturo Vidal, 32. Mchezaji huyo inasemekana kwamba yuko tayari kuhama ikiwapo timu hiyo itambadili kocha wake sasa Steve Bruce na mahala pake kuchukuliwa na Max Allegri. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Mshambuliaji wa Uhispania Pablo Mari, 26, anataka kufanya makubaliano yake ya uhamisho wa mkopo kwa Arsenal kutoka Flamengo kuwa wa kudumu msimu ujao. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa France Kylian Mbappe, 21, thamani yake itapungua hadi euro milioni 35 kutoka 40 baada ya virusi vya corona. (AS)

Kylian Mbappe will cost a measly £35m after coronavirus with ...

Arsenal na Everton ziko tayari kumsajili mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Le10 Sport – in French)

Arsenal imewasiliana na Reims kwasababu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa Axel Disasi, 22. (Goal)

Liverpool imeelekeza macho yake kwa kiungo wa kati wa Inter Milan na Croatia Marcelo Brozovic, 27. (Libero, via Mirror)

Hatahivyo, Liverpool haijawasiliana na RB Leipzig kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa Ujerumani, 24, Timo Werner. (General Anzeiger – in German)MbappeKylian Mbappe

Barcelona inataka kumuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho – ambaye kwasasa yuko kwa mkopo Bayern Munich – kukiwa na matumiani kwamba kutapatikana mnunuzi anayemuhitaji mchezaji huyo, 27, kutoka ligi ya Primia. (Goal)

Liverpool itapunguza gharama ya winga wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, kwasababu ya janga la virusi vya corona. (Football Insider)

Tetesi za Jumamosi

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda akahamia Real Madrid, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa Senegal Keita Balde, ambaye pia aliongeza kuwa Mane, 28, Pia anaweza kusalia Anfield “milele”. (AS, in Spanish)

Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 28, kutoka Paris St-Germain.Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane(Aliye na mpira) huenda akahamia Real MadridMshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane(Aliye na mpira) huenda akahamia Real Madrid

Miamba hao wa soka wa Uhispania wako tayari kuwajumuisha Samuel Umtiti, Ousmane Dembele na Jean-Clair Todibo katika mkataba huo baada ya hali yao ya kifedha kuathiriwa na Jana la coronavirus. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya Manchester United na huenda akawa kiongozi wa klabu hiyo, kwa mujibu wa mwandishi wa michezo wa Uhispania Guillem Balague. (Express)

Kipa wa muda mrefu wa Juventus Gianluigi Buffon, 42, amekubali kurefusha mkataba wake katika klabu hiyo. Hii itakuwa msimu wa 19 kwa mtaliano huyo Turin. (Tuttosport, in Italian)

The post Dortmund kumuongezea mshahara Jadon Sancho, virusi vya corona vyashusha thamani ya dau la Mbappe appeared first on Bongo5.com.