Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro @Lengai_ole_sabaya Ameamuru kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa kwa Afisa Manunuzi na ugavi wa halmashauri ya wilaya hiyo ndg Sabiano wambura.

Mkuu wa wilaya @lengai_ole_sabaya amefikia uamuzi huo baada ya afisa ugavi huo kushindwa kupeleka vifaa vya ujenzi katika kituo cha Afya ambapo serkali kuu ilileta Tsh mil 30 toka mwaka jana mwezi wa nane kupelekea wananchi kukosa huduma muhimu za afya.

Sambamba na hilo mkuu huyo wa wilaya amemuelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kinidham ikiwepo kumsimamisha kazi wakati hatua hizo zikiendelea.

Baada ya kutoa maagizo hayo Dc @lengai_ole_sabaya alielekeza kituo hicho cha afya kikamilike ndani ya siku 14.

By Ally Juma.

The post DC Ole Sabaya aamuru kusimamishwa na kuchunguzwa Afisa manunuzi wa Halmashauri, Aeleza Sababu hizi – Video appeared first on Bongo5.com.