Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amethibitisha wagonjwa kulazimisha kutaka kuondoka katika Hospitali ya Mkoa ya Rufaa, Amana na kurejea nyumbani.

Amesema, kuna wagonjwa ambao walifika pale wakawa wanasema wao wanaona hawaumwi sana hivyo wakataka waruhusiwe kuondoka

Amesema hana hakika sana kama kulitokea vurugu hospitalini hapo ila ni ile hali ya Wagonjwa hao kupiga kelele wakitaka waruhusiwe

Aidha, kuhusu wagonjwa kutoroka na kupanda magari ya Umma kurudi nyumbani amesema hili hana taarifa na bado wanaifuatilia kwa Askari waliopo hapo kujua kama kuna waliotoroka ni wangapi na wamekwenda wapi

Amesema kama kutakuwa na waliotoroka basi watafuatiliwa maana wanajulikana walipochukuliwa iwapo asipokuwepo Hospitalini basi ataenda kufuatiliwa alipochukuliwa

Ameongeza kuwa, kwa sasa hali ni shwari katika hospitali hiyo na kuwataka wagonjwa waliopo eneo hili kufuata utaratibu na kama wako salama wataruhusiwa kuondoka

Amesema “Napenda kuwaambia wananchi watulie na wasikilize Serikali inawaambia nini kwasababu mgonjwa akifika pale anaangaliwa kama yupo salama ataruhusiwa la sivyo atabaki hapo”

The post DC Mjema amethibitisha wagonjwa kulazimisha kutaka kuondoka kituo cha wagonjwa wa corona Amana appeared first on Bongo5.com.