Daktari aliyekutana na rais wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita alipokuwa akizuru hospitali moja huko Moscow, amepatikana na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo, Televisheni ya serikali, Rossiya 24, imeripoti leo Jumanne.
 
Rais wa Urusi alizuru hospitali ya Kommunarka Jumanne wiki iliyopita ambapo alikutana na daktari mkuu wa hospitali hiyo Denis Protsenko. 

Wote wawili hawakuwa wamevaa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa mazungumzo yao.

"Hali ni shwari," ofisi ya rais wa Urusi (Kremlin) imesema, ikinukuliwa na shirika la habari la RIA, huku ikikumbusha kwamba Vladimir Putin huwa anafanyiwa vipimo mara kwa mara.