Klabu ya Real Madrid imeahirisha mipango yake ya kumsajili mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris Saint-Germain mpaka 2021 kutokana na janga la virusi vya corona. (AS)
Klabu za Arsenal, Chelsea na Celtic wanamuwania mshambuliaji kinda wa Middlesbrough na timu ya taifa ya chini ya miaka 17 ya Jamhuri ya Ireland Calum Kavanagh, 16. (Sun)
Liverpool imejiunga na msururu wa klabu zinazovutiwa na kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille ya Ufaransa Boubakary Soumare, 21. Klabu za Real Madrid, Manchester United, Chelsea na Newcastle pia zinamuwania mchezaji huyo. (Sport)
Wakati huo huo, Liverpool wanataka kumsajili beki raia wa Brazili Diego Carlos, 27, kutoka klabu ya Sevilla. (Marca)
Klabu ya AC Milan imetuma maombi ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester City David Silva, 34. Kiungo huyo raia wa Uhispania anamaliza mkataba wake na City mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport – in Italian)
AC Milan pia wanaandaa pauni milioni 35 ili kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24. (Corriere Dello Sport – in Italian)
Manchester United bado wanahangaika kutafuta klabu itakayomnunua mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 31, kwa kuwa hataki kupunguza mshahara wake. Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye yupo kwa mkopo Inter Milan, bado yungali na miaka miwili mpaka mkataba wake na United uishe. (Standard)
Winga Yannick Bolasie, 30, anatarajiwa kurejea Everton kutoka Sporting Lisbon mwishoni mwa msimu kulingana na wakala wake. lakini miamba hiyo ya Ureno haitaki kumsajili moja kwa moja. (Record – in Portuguese)
Everton pia pia wanamnyemelea mshambuliaji raia wa Brazil mwenye jina kama lao Everton Soares, 24. Hata hivyo, mshambuliaji huyo mkataba wake na klabu ya Gremio unaelekeza auzwe kwa dau la si chini ya pauni milioni 104. (Mirror)
Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez,
Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka klabu ya Inter Milan lakini wanakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid na Manchester City. (Marca)
Klabu ya Wolves haitamuuza Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70 huku winga huyo akihusishwa na mipango ya kuhamia Liverpool. (Football Insider)
Arsenal wanalenga kumsajili beki wa Athletic Bilbao Unai Nunez, 23, kama kipaumbele chao kwa usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa Uhispania ana kifungu cha mkataba kinachoelekeza kuuzwa kwa euro milioni 30. (La Razon – in Spanish)
The post Corona yaaribu mipango ya Madrid kwa Kylian Mbappe, Liverpool kumsajili Carlos wa Brazili, wengine sokoni appeared first on Bongo5.com.