Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelazwa Hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya afya yake kuzorota kutokana na Virusi vya Corona.

Coronavirus: Boris Johnson kept in hospital for coronavirus ...

Ofisi yake imesema kwamba alipelekwa katika chumba hicho kutokana na ushauri wa madaktari wake na kwamba alikuwa akipokea uanagalizi wa karibu sana.

Bwana Johnson amemtaka waziri wa maswala ya kigeni Dominic Raab kumsaidia pale atakapoweza, msemaji alisema.

Waziri mkuu mwenye umri wa miaka 55 alilazwa katika hospitali ya St. Thomas akiwa na dalili kali za virusi vya ugonjwa huo siku ya Jumapili jioni.

Malkia amekuwa akiarifiwa kuhusu afya ya Johnson kulingana na kasri la Buckingham.

Mwandishi wa maswala ya kisiasa wa BBC, Chris Mason alisema kwamba Waziri Mkuu alipatiwa oksijen baadaye siku ya Jumatatu mchana kabla ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Alisahamishwa kama hatua ya kuchukua tahadhari ili awekwe karibu na mashine ya kumsaidia kupumua , alisema mwandishi huyo.

Mapema Jumatatu ujumbe uliandikwa kwenye mtandao wa Twitter ukiashiria kwamba anaendelea kupata afueni.

Tuizuru ofisi ya waziri mkuu na maambukizi ya Virusi vya Corona mpaka sasa

March 10: Waziri wa afya Nadine Dorries alikua mbunge wa kwanza kupima virusi vya ugonjwa huo, muda mfupi baada ya kuhudhuria mapokezi ya Mtaa wa Downing.

March 27: Waziri mkuu Boris Johnson na Katibu wa Afya Matt Hancock wote wawili wakaachia video zao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakisema wana uambukizo wa corona na wanajitenga.Saa kadhaa baadaye , afisa mkuu wa matibabu Profesa Chris Whitty alifichua kuwa alikuwa akijitenga na dalili.

March 30: Mshauri mkuu wa waziri mkuu Dominic Cummings naye aliarifiwa kujitenga binafsi na uambukizo wa virusi hivyo

April 2: Matt Hancock anarudi kazini baada ya watu saba kufa wakati alipokuwa kwenye karantini akiwa na ahueni kubwa.

April 3; Boris Johnson aachia video akiwa kwenye ghorofa yake ya Namba 11 akisema anaendelea kujitenga kwani bado anapata homa na inapanda.

April 4: Carrie Symonds, ni mchumba wa waziri mkuu Borisi ambaye kwa sasa ni mjamzito naye amekuwa akijitenga katika chumba chake huko Camberwell.

April 5: Waziri mkuu apelekwa hospitalini ‘kwa tahadhari’.

April 6: Ofisi ya waziri mkuu yakataa kutoa taarifa wazi zaidi kumhusu na msemaji wake asema bado ana kikohozi cha ‘kuendelea’ na joto mwilini

April 7; Waziri mkuu Boris Johnson ahamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya St Thomas na nafasi yake kukaimiwa na waziri wa Mambo ya nje Dominic Raab.

The post CORONA: Waziri Mkuu Uingereza apelekwa chumba cha wagonjwa Mahututi appeared first on Bongo5.com.