Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuongezeka kwa wagonjwa wapya watano wa virusi vya Corona nchini, aidha mapema leo wagonjwa wapya wawili pia wametangazwa Zanzibar na kufanya idadi ya wagonjwa nchini kufikia 32. Wagonjwa wote wapya ni Watanzania.

Waziri Ummy pia ametangaza vifo vingine viwili na kufanya idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huu kufikia watatu. Waliofariki wote ni wanaume wenye umri wa miaka 51 na 57.

The post Corona Tanzania: Vifo vitatu, wagonjwa wafikia 32 appeared first on Bongo5.com.