Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi, Mawaziri wake pamoja na Wabunge wote wa Bunge la Nchi hiyo, wamewekwa karantini kwa siku 14 baada ya muuguzi aliyewapima dalili za virusi vya Corona viongozi hao na yeye kugundulika kuwa ni mgonjwa COVID – 19.

A Conversation With Mokgweetsi Masisi - YouTube

Hatua hiyo ili jiri baada ya Rais wa taifa hilo, Mokgweetsi Masisi kuhitisha kikao maalumu cha bunge lenye jumla ya wabunge 65 kikiongozwa na mkuu huyo wa nchi kutoka chama cha Botswana Democratic Party ili kujadili hatua ya kuongeza muda wa hali ya hatari kwa taifa hilo ambapo sasa muda huo umeongezwa hadi mwezi Oktoba.

Lakini wakati wabunge hao wakiwa hapo inadaiwa walikutana na muuguzi aliyekuwa na virusi vya corona, ambaye yeye alihusika kuwapima corona viongpozi hao akiwa katika majukumu yake Bungeni, ambapo vipimo vyake vilionyesha kuwa na COVID-19.

Hivyo wabunge wote watakuwa karantini kwa siku 14, Kwa mujibu wa spika wa wa bunge la Botswana, Phandu Skelemani amesema kuwa wabunge hao wanaweza kutengwa wakiwa nyumbani ama kuhamishiwa sehemu maalum zilizotengwa itategemea na wahudumu wa afya watakavyopendekeza.

The post Corona: Rais na wabunge wote Botswana wawekwa Karantini appeared first on Bongo5.com.