Kiungo wa Manchester United Bruno Frenandez amefunguka mengi sana baada ya kufanyiwa mahojiano na kusisitiza kuwa ataweza kucheza kando ya mchezaji yeyote wa United kwa sababu anahisi mtindo wake wa kucheza ni wa kipekee san.”Nadhani mimi ni mchezaji tofauti na wengine,”
Kila mtu ana mtindo wake tofauti wa kucheza, labda mimi hujitolea zaidi nikiwa uwanjani, labda wachezaji wengine wana namna ya kucheza, labda mimi hupiga mashuti zaidi, wachezaji wengine hufanya tackles sana lakini mimi sifanyi, wachezaji wengine hufanya mbwembwe zaidi, kila mtu ni tofauti kwenye uchezaji wake kamwe hatuweza kucheza sawa.
“Mimi ni mchezaji ambaye hupenda kujitolea zaidi, pia napenda kutoa pasi za mwisho na jaribu kutoa msaada zaidi kwa wachezaji wenzangu kwa hivyo ninahitaji kujitolea zaidi.
Mbali na hilo Bruno aliongelea kuhusu michezo iliyobaki na nafasi ya pogba
“Kwa michezo hii tisa ya ligi iliyobaki, itakuwa kama tumekuwa na mchezaji mwingine mpya kwa sababu msimu huu hatujamuona Paul Pogba sana uwanjani,”
“Tunaweza kuzungumza juu ya kuleta wachezaji wapya lakini hatujaona kabisa Pogba akicheza kwa kufurahia labda kwa sababu moja au nyingine labda akirejea itaonekana nafasi ya kuletwa mchezaji mwingine.
“Alikuwa na majeraha, lakini wakati huo huo mimi namtarajia kumuona akirudi tupeane changamoto mpya tunatazamia kuona ushirika mzuri lakini pia huo ushirikiano unaileta nini klabu kwa sababu Paul anataka kucheza bora zaidi na kuonyesha matunda yake baada ya kuwa nje Kwa kweli ni kitu cha kutarajia. ” “Namjua Pogba tangu yuko Juve kwa sababu nilicheza naye huko, Ni ngumu kupata mchezaji kama yeye ni hodari uwanjani kiufundi. Niamini, ni ngumu sana kumkaba Paul”
By Ally Juma.
The post Bruno Fernandes kuhusu Pogba “Namjua tangu yuko Juve, Ni ngumu kupata mchezaji kama yeye ni hodari kiufundi, Ngumu sana kumkaba” appeared first on Bongo5.com.