Idadi ya visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona visiwani Zanzibar imeongezeka na kufikia 9, baada ya hii leo kutangazwa visa vipya viwili, ambapo wote ni wa Tanzania na hawana historia ya kusafiri nje ya nchi siku za hivi karibu na kwamba wote kwa pamoja walianza na homa, mafua na kifua.
Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 10, 2020, na Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed, na kusema kuwa mgonjwa wa kwanza ana umri wa miaka 33 na ni mkazi wa Mwanakwerekwe, ambapo aliripotiwa akiwa na homa kali, mafua na kifua.
"Mgonjwa wa pili ana miaka 24, mkazi wa Mtendeni na wagonjwa hawa wote hawana historia ya kusafiri nje ya nchi hivi karibuni, aidha Wizara inaendelea kuwafuatilia wengine 86 waliowahi kukutana na hawa wagonjwa, pia kuna watu 252 waliorudi kutoka nje ya Tanzania wamewekwa Karantini Unguja na Pemba" amesema Waziri wa Afya Zanzibar