Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wengine  2 wa Corona hapa nchini  wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufika 5 huku kifo kikiwa ni kimoja.

Amesema kati ya wagonjwa hao, Dar es Salaam - 1 na Arusha - 1.  Hivyo sasa Mkoa wa Arusha hauna mtu mwenye maambukizi ya COVID19. 

Waziri Ummy amewataka Watanzania waendelee kuzingatia maelekezo ya Wataalam wa Afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko na misongamano  isiyo ya lazima