Moja kati ya picha iliyo-trend mitandaoni ni hii ambayo inamuonesha Bibi wa miaka 94, ambaye ameshika bango ambalo linaeleza kuwa anahitaji bia zaidi, baada ya kufungiwa ndani “Lockdown” wakati wa kipindi hiKi cha ugonjwa wa Corona.

Bibi aliyeshika bango akitaka apewe bia zaidi

Bibi huyo ambaye amejulikana kwa jina la Olive Veronesi, kutokea Mji wa Pittsburgh, Pennsylvania iliyopo Marekani, amefanikiwa kupata anachokitaka baada ya kuchangiwa makopo 150 ya bia.

Kwa mujibu wa CBS  Pittsburgh, Bibi huyo Olive Veronesi amesema anapenda sana bia kwa sababu ina virutubisho na lazima anywe kila ifikapo usiku.

Nilikuwa nimebakiwa na makopo 12 ya bia, lazima niwe na bia kila ifikapo usiku, halafu unajua bia ina vitamini na ni nzuri kwako kama hautazidisha” amesema Bibi huyo.

By Ally Juma.

The post Bibi wa miaka 94 akiwa lockdown aonyesha bango likisomeka “Nahitaji bia zaidi, Nimebakiwa na makopo 12 tu” appeared first on Bongo5.com.