Wimbi la pili la nzige linatarajiwa kusababisha uharibifu mkubwa mashariki mwa Afrika, miezi miwili baada ya kundi la wadudu hao hatari kuvamia mimea muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa mlipuko wa virusi vya corona.

”Inaonekana kwamba wale waliokwepa Covid 19 watakabiliana na Locust 19”, alisema Akiwumi Adesina rais wa benki ya maendeleo barani Afrika na waziri wa zamani wa kilimo.

Kitu cha mwisho ambacho Afrika inahitaji sasa ni ukosefu wa chakula.

Nzige tayari wamevamia nchini Somalia, Ethiopia, Kenya, Uganda, Ethiopia na Sudan Kusini mara moja mwaka huu, mwezi Januari na Februari.

”Sasa makundi hayo ya nzige baada ya kuzaa mayai ,yanaweza kuwa mara 20 zaidi ya yalivyokuwa”, amesema mtaalam huyo.

”Mara ya mwisho Kenya kuathiriwa na uvamizi wa nzige wa kiwango kama hiki ni miaka 70 iliopita wakati ilipokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza’, alisema Keith Cressma, mtaalamu wa utabiri wa nzige katika shirika la chakula na kilimo katika Umoja wa mataifa FAO.

Uvamizi huo unahatarisha kusababisha tatizo la chakula ambalo tayari limekuwa likitarajiwa katika upembe wa Afrika.

Asilimia 40 ya watu milioni 160 katika eneo hili hawapati lishe bora, kulingana na FAO.

Nzige waliovamia maeneo ya Somaliland wafukuzwa kwa kufyatuliwa risasi

Licha ya kuwepo kwa masharti ya usafiri kukabiliana na virusi vya corona, wataalamu wa kimataifa tayari wamejiandaa kusaidia juhudi za kukabiliana na wadudu hao kupitia mikakati ya kunyunyuzia dawa angani na ardhini.

”Ukosefu wa uzoefu na vifaa umeathiri juhudi za kuwaangamiza wadudu hao mapema mwaka huu” , alisema , hatua iliowapatia wadudu hao waharibifu uwezo wa kuzaa mayai mchangani na kuzaana zaidi.

Bwana Cressman alisema kwamba kizazi hiki kitasababisha uharibifu mkubwa , sio tu kwasababu ya idadi yao, kwa sababu wadudu hao walikuwa wanaanza kuruka, na kula mwanzo wa msimu wa kupanda mimea.

”Wakulima wataahirisha kupanda mimea la sivyo nzige watakula mbegu zilizopandwa ardhini”, alisema. ”Suala ambalo ni hatari”.

Makundi makubwa ya nzige yanaweza kuwa na ukubwa wa kilomita moja mraba.

Mwanamume akinyunyizia dawa EthiopiaUnyunyiziaji wa dawa umekuwa ukifanyika katika mataifa mengi, ikiwemo Ethiopia na Kenya

Shirika la chakula na kilimo FAO , limefanikiwa kuchangisha takriban $120m kukabiliana na tatizo hilo , hatua ambayo itasaidia juhudi za serikali katika mataifa yalioathirika.

”Kundi la kwanza la wadudu hao waharibifu liliwasili wakati wakulima walipokuwa wanakaribia kumaliza mavuno”, alisema Cyril Ferrand kiongozi wa ujasiri dhidi ya wadudu hao Afrika katika shirika la FAO.

Hivyo basi kulikuwa na uharibifu mdogo katika mimea.

”Hatahivyo , kuanzia mwanzo wa msimu wa mvua, mimea mipya ilimaanisha kwamba wimbi la pili lilikuwa tayari linafanya uharibifu katika mimea inayoanza kuota”, alisema.

”Nzige hao wa jangwani hula kila kitu chenye rangi ya kijani lakini mimea ilioota ndio chakula wanachokipenda. Na wao hula kila kitu”, alisema.

Wao husafiri kwa kutumia upepo na kuelekea kaskazini katika taifa la Sudan kufikia mwezi Juni na Julai na baadaye kuelekea katika eneo la Sahel.

The post Benki ya maendeleo Afrika yaeleza Afrika mashariki, kukumbwa na wimbi la Nzige kwa mara ya pili appeared first on Bongo5.com.