Kikosi cha Miamba ya soka nchini Ujerumani, Bayern Munich kinatarajiwa kurejea uwanjani kuanza kufanya mazoezi yake hii leo siku ya Jumatatu kwa mara ya kwanza tangu Bundesliga kusimamisha shukhuli zote za kimichezo kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Ligi hiyo ya Ujerumani ilipendekeza klabu zake kutofanya mazoezi mpaka ifikapo Jumapili ya Aprili 5, na vinara hao wa Bundesliga wanatarajia kuanza kwa wachezaji wachezaji wache kwanza.
“Mazoezi yataanza pasipo kuhudhuriwa na wanachama, ili kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona. Mashabiki wa FC Bayern wanaombwa kufuata muongozo na taratibu mamlaka na hivyo basi tafadhali usifike kwenye uwanja wa mazoezi wa FC Bayern,” maelezo yaliotolewa na klabu hiyo.
Hata hivyo ligi hiyo ya Bundesliga bado imesimamishwa hadi AprilI 30, hiyo ni kufuatia na maamuzi ya Mkutano wa vilabu uliyofanyika siku ya Jumanne ya wiki iliyopita.
The post Bayern Munich kurejea Uwanjani hii leo appeared first on Bongo5.com.