Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, ametangaza kumuunga mkono aliyekuwa Makamu wake Joe Biden kupeperusha bendera ya chama cha Democratic kumenyana na rais Donald Trump wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Mpinzani mkuu wa Biden, Bernie Sanders alijondoa katika kinyanyanyiro cha kutafuta bendera ya chama hicho katika dakika za lala salama.

Jumanne wiki hii Makamu wa zamani wa rais wa Marekani Joe Biden, mgombea wa uchaguzi wa Novemba, alipokea rasmi uungwaji mkono kutoka kwa mpinzani wake mkuu katika chama cha Democratic, Bernie Sanders.

Hii ni hatua inampa nafasi ya moja kwa moja Joe Biden kuchuana dhidi ya rais Donald Trump anayemaliza muda wake katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu.