Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID -19 katika mataifa ya Ulaya vimepindukia 100,000. Bara la Ulaya ndio limeathirika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mabara mengine duniani.

Spanien Corona-Pandemie | Fast 98.000 Corona-Todesfälle in Europa (picture-alliance/AP Photo/M. Fernandez)

Takriban watu 2,281,334 wamepata maambukizi ya virusi vya corona hadi sasa duniani kote. Mataifa ya Ulaya yamekabiliwa na vifo vya  watu 100,510 idadi hiyo ikiwa karibu theluthi mbili ya watu wote 157,163 waliofariki duniani kote kutokana na COVID -19 kwa mujibu shirika la habari la Ufaransa AFP.

Hata hivyo karibu robo ya vifo vilivyotokea ulimwenguni kote vimetokea nchini Marekani ambapo watu wapatao 38,000 wamekufa, kulingana na chuo kikuu cha John Hopkins.

Zaidi ya watu bilioni 4.5 wanaendelea kubaki majumbani kama sehemu ya juhudi zinazochukuliwa kwa hiari au za lazima ili kupunguza kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Japan, Mexico, Uhispania, Ufaransa, na Uingereza ni kati ya nchi ambazo zimeweka hatua hizo au hata kurefusha muda wa watu kubakia majumbani. Uswizi, Denmark na Finland zimetangaza kwamba maduka na shule zitafunguliwa tena kuanzia wiki ijayo.

Vyanzo:/AFP/DW

The post Bara la Ulaya laathirika zaidi na Virusi vya Corona, vifo kutokana na COVID-19 vyapindukia 100,000 appeared first on Bongo5.com.