Msanii wa muziki wa bongo Fleva Babalevo ameweka wazi nia yake ya kusainiwa katika lebo mbili kubwa za muziki nchini Tanzania ambazo ni WCB iliyopo chini ya Diamond Platnumz na KINGS MUSIC iliyopo chini ya Alikiba.

Babalevo amesema kuwa ” Diamond akitaka kukusaini siwezi kukata kuingia WCB sio Diamond tu hat Alikiba ni bahati ya Mtende hiyo”

Babalevo aliongeza kuwa “kukutwa kwenye muziki sio tija shida ni kuwa na hela, Unajua kuna utofauti watu wanatakiwa wajue kuna msanii mkubwa na msanii mkongwe, kuna mtu anang’anga’nia tu mi msanii mkubwa kwa sababu tu alianza kuimba zamani, wewe ni mkongwe sasa hivi wasanii wakubwa wanajulikana, Ukitaka kutaja wasanii wakubwa utawataja ambao ni Diamond Platnumz, Alikiba, Rayvanny na Harmonize hao ndio wasanii wakubwa kwenye hii nchi wanafanya kazi kubwa zinaonekana lakini sisi wengine ni wakongwe tuna ukubwa gani vitu haviendi”

View this post on Instagram

Babalevo "Kusainiwa na Diamond au Alikiba ni bahati ya mtende, Wasanii wengine wamekalia kusema wao wakubwa huku hawana mafanikiwa yoyote kumbe ni wakongwe" Msanii wa muziki wa bongo Fleva Babalevo ameweka wazi nia yake ya kusainiwa katika lebo mbili kubwa za muziki nchini Tanzania ambazo ni WCB iliyopo chini ya Diamond Platnumz na KINGS MUSIC iliyopo chini ya Alikiba. @officialbabalevo amesema kuwa " Diamond akitaka kukusaini siwezi kukata kuingia WCB sio @diamondplatnumz tu hata @officialalikiba ni bahati ya Mtende hiyo" Babalevo aliongeza kuwa "kukutwa kwenye muziki sio tija shida ni kuwa na hela, Unajua kuna utofauti watu wanatakiwa wajue kuna msanii mkubwa na msanii mkongwe, kuna mtu anang'anga'nia tu mi msanii mkubwa kwa sababu tu alianza kuimba zamani, wewe ni mkongwe sasa hivi wasanii wakubwa wanajulikana, Ukitaka kutaja wasanii wakubwa utawataja ambao ni @diamondplatnumz , @officialalikiba , @rayvanny na @harmonize_tz hao ndio wasanii wakubwa kwenye hii nchi wanafanya kazi kubwa zinaonekana lakini sisi wengine ni wakongwe tuna ukubwa gani vitu haviendi" (📹 via HZB) written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

By Ally Juma.

 

 

The post Babalevo “Kusainiwa na Diamond au Alikiba ni bahati ya mtende, Wasanii wengine wamekalia kusema wao wakubwa huku mambo hayaendi kumbe ni wakongwe” – Video appeared first on Bongo5.com.