Askari wa Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha KIA Hai, Kilimanjaro, Sajent Juma Ango anadaiwa kuuawa na Watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa mtaroni.

Kaimu RPC Kilimanjaro James Manyama amesema mwili wa Askari huyo aliyekuwa kitengo cha upelelezi kituo cha polisi KIA umekutwa ukiwa na majeraha kadhaa katika sehemu za kichwani na usoni kando ya mgahawa wa chakula uliopo eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema April 14 saa mbili asubuhi watu waliokuwa wakifyeka majani kandokando ya Barabara Kuu ya Arusha Moshi ndio waliouona mwili huo na kutoa taarifa polisi.

Sabaya alibainisha kuwa mwili wa askari huyo ulikutwa ukiwa na jeraha kubwa kisogoni na kwamba alikuwa amepigwa na kitu chenye ncha kali.