Inter Milan inataka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29, kwa kumbadilishana na mshambuliaji Lautaro Martinez ikiwa Barcelona itamnyakua kiungo huyo wa Argentina wa miaka 22 kutoka kwao. (La Gazzetta dello Sport, via Marca)

Inter Milan inamtaka mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann

Barcelona itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 20, kutoka Real Sociedad wakimkosa Martinez. (Marca)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, 29, ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaolengwa na Real Madrid. (AS, via Mail)N'Golo Kante

N’Golo Kante, 29, ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaolengwa na Real Madrid

Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anasema mshambuliaji wa Spurs Harry Kane hatahamia Manchester United lakini nahodha huyo wa England “huenda akapendelea” kujiunga na Barcelona ama Real Madrid “siku moja”. (Talksport)

Arsenal na Chelsea watapewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Barcelona, Philippe Coutinho msimu huu wa joto, huku Bayern Munich wakijiandaa kubadili mkataba wake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Sun)

Philippe CoutinhoArsenal na Chelsea kupewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Barcelona Philippe Coutinho

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez lakini iko tayari kulipa £70m kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa paundi milioni 132. United wanatarajiwa kuongeza marupurupu yake kwa kati ya £115,000-a- hadi karibu £200,000 kwa wiki. (Sun)

Wakala wa kiungo wa kati wa Ajax midfielder Donny van de Beek, andasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi wa miaka 22- amabye anahusishwa na tetesi ya kuhamia Real Madrid na Manchester United,ananyatiwa na “klabu kadhaa. (Voetbal International, via Metro)Sergio AgueroSergio Aguero anatakiwa na klabu yake ya zamani ya Independiente

Klabu ya zamani ya mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, Independiente imeongeza juhudi ya kutaka kumrejesha tena nyota huyo Argentina wa miaka 31 katika klabu hiyo. (Mirror)

Mashambuliaji wa Italia Lorenzo Insigne, 28, anajiandaa kurefusha mkataba wake na Napoli hadi 2025. (Calciomercato)

The post Arsenal yajipima ubavu kwa Coutinho, Real Madrid kusaka saini ya N’Golo Kante wengine sokoni Ulaya appeared first on Bongo5.com.