Wakati huu ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika yameweka marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corano, bila shaka wanyamapori wamegundua kuwa watu wameondoka.

Katika moja ya hifadhi kubwa ya wanyama pori barani Afrika Simba wameamua kuchukua fursa hiyo kujipumzisha barabarani.

Msimamizi wa hifadhi ya Kruger nchini Afrika Kusini Bw. Richard Sowry siku ya Jumatano, alipokuwa katika operesheni ya kikazi alikutana na kundi kubwa la Simba waliokuwa katika usingizi mzito katikati ya barabara tofauti na hali ya kawaida ambapo watalii au wageni ndio wengi barabarani.

Lakini hifadhi ya Kruger, kama ilivyo hifadhi nyingine zimefungwa tangu Machi 25, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na virusi vya corona.

Walinzi wa hifadhi hiyo wanasema kwa kawaida simba huwa wanaonekana barabarani nyakati za usiku.

Picha hii ilipigwa vipi?

Bw Sowry alikuwa anaendelea na shughuli ulinzi kuangalia kama wawindaji pori hawavamii wanyama katika muda wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.

Simba ambaye ana umri mkubwa zaidi ni miaka 14, hivyo wamezoea kuona magari.Kwa kawaida bwana Sowry huwa anawaona simba wakiwa wamelala katika barabara za hifadhi wakati wa usiku katika majira ya baridi.

Lions in Kruger National ParkHaki miliki ya pichaRICHARD SOWRY/KRUGER NATIONAL PARK

Wakati alipokuwa akiendesha gari karibu na hifadhi majira ya mchana siku ya Jumatano, aliwaona samba wakiwa wamejaa barabarani wakiwa wamelala jambo ambalo si la kawaida,hivyo ilimbidi arudi nyuma kama mita tano na kuwangalia.

Wakati akipiga picha kwa simu yake, Simba hao hata walikuwa hawajishughulishi kwanza wengi walikuwa katika usingizi mzito.

“Simba wamezoea watu wakiwa kwenye magari,” alieleza.

“Wanyama wote huwa wanaogopa watu wakiwa wanatembea, hivyo kama ningetembea wasingeweza kuniruhusu.”

Kitu ambacho askari pori hawataki ni kuona simba kudhani kuwa barabara ziko salama kwa wao kupumzika.

Lions in Kruger National ParkHaki miliki ya pichaRICHARD SOWRY/KRUGER NATIONAL PARK

Marufuku dhidi ya Corona imeathiri hifadhi za wanyama kiasi gani?

Nyakati hizi simba wanakuwa wanaonekana wakiwa maeneo ya wazi kama mbwa pori katika hifadhi lakini kwa upande mwingine bwana Sowry anadhani kuwa marufuku ya kuzuia watu kutoka nje haiweza kuleta mabadiliko makubwa katika tabia za wanyama pori.

“Hifadhi ya Kruger ni eneo la pori sana,” alisema. “Limekuwa eneo la wanyama pori na litaendelea kuwa eneo la wanyama pori.”

 

By Ally Juma.

The post Afrika Kusini: Yaelezwa Simba wavinjari na kupumzika barabarani baada ya watu kuzuiliwa kutoka kisa Corona appeared first on Bongo5.com.