Video mpya ya wimbo ‘Unanikosha’ ya muiambaji hodari @marioo_tz imetoka siku ya leo huku mapokezi yakiwa ni makubwa sana.

Mpaka video hiyo iliyoandaliwa na muongozaji mkongwe wa video za muziki nchini Tanzania, @adamjumanxl inafanya vizuri kupitia mtandao wa kipindi cha masaa 12 toka itoke.

Mashabiki kupitia mitandao ya YouTube na Instagram wameonekana kumkubali zaidi muongozaji wa video hiyo kwa madai ameutendea haki wimbo huo.

Muongozaji huyo mwaka huu amenekana kuja kwa kasi kwa kufanya video nyingi za muziki tofauti na mwaka mmoja uliopita ambao alikuwa anafanya project moja na kupumzika.

Adam ambaye kwa sasa yupo busy na chuo chake cha Adam Juma Film Academy, ameongoza video kama Bao ya Kassim Mganga, Unanikosha ya Marioo, Ivinty ya Ado akiwa na Mr Blue, Gimmie Love ya Bytar na Maua Sana pamoja na nyingine nyingi.

Je wewe una mtazamo gani na Adam Juma ambae ameonekana kuufungua mwaka 2020 vizuri ?. Kuangalia full video ya Unanikosha ingia kwenye bio ya Marioo.

The post Adam Juma arudi kwa kasi, angalia alichokifanya kwenye Unanikomesha ya Marioo (Video) appeared first on Bongo5.com.