Taarifa potofu juu ya Coronavirus zimesambaa katika mitandapo na wataalamu wanatoa wito kwa umma kutumia “taarifa safi”. lakini je ni vipi unavyoweza kufanya ili kuzuwia kusambaa kwa taarifa mbaya ?

News logo

1. Tulia na ufikirie kwanza

Unataka kuisaidia familia na marafiki na kupata taarifa za uhakika. Kwahivyobasi unapopokea taarifa mpya ya ushauri iwe kwa -barua pepe, WhatsApp, Facebook au Twitter – huenda unaweza kuutuma haraka kwao.

Lakini wataalamu wanasema kuna jambo moja unaloweza kulifanya kuzuwia taarifa za uzushi ni kutulia na kufikiria kwanza.

Kama unawasiwasi wowote, tulia na uuangalie zaidi.

Graphic shows a mobile phone with "fake news" on it being cleaned by tiny cleaners.

2. Angalia chanzo chake

Kabla haujautumwa kwa watu wengine, jiulize maswali kadhaa ya kimsingi kuhusu ni wapi taarifa imetoka.

Ufikirie zaidi kama chanzo chake ni “rafiki wa rafiki ” au ” jirani ya mfanyakazi mwenzake na shangazi yangu”.

Miongoni mwa taarifa gushi zilizochunguzwa na BBC ilikua ni jinsi ujumbe uliotumwa na ”mjomba wa mtu fulani mwenye shahada ya juu uliokua feki ulivyosambaa kwa kiwango kikubwa.

Baadhi ya mae;ezo katika ujumbe huo yalikua yalikua sahihi – baadhi kwa mfano , yalihusu ushauri kwa watu kunawa mikono kupunguza kusambaa kwa virusi. Lakini maelezo mengine yalikua ni ya madhara, ambayo yalitoa ushauri kuhusu jinsi ya kutambua ugonjwa.

” Chanzo sahihi zaidi ya habari ni taasisi za afya kama vile wizara ya afya, Shirika la Afya Duniani, na vituo vya kitaifa vya udhibiti wa ugonjwa

Illustration showing sharing of information to lots of usersTaarifa gushi zinaweza kusababisha madhara zaidi kuliko kumsaidia mtu unayemshirikisha ujumbe, wanasema wataalamu

Wataalamu wanaweza kutoaminiwa , lakini ni bora zaidi kuliko mtu usiyemfahamu au ndufu anayekutumia ujumnbe katika WhatsApp.

3. Jiulize je unaweza kuwa ni feki?

Muonekano unaweza kukudanganya

Unawezekana kutumia akaunti au nembo rasmi na mamlaka, mkiwemo BBC News na BBC News Swahili na serikali. Screenshoti pia inaweza kubadilishwa na kufanywa ionekane kama taarifa iliyotoka katika taasisi ya umma ya kuaminika.

Angalia na hakiki kurasa na tovuti. Kama hauwezi kupata taarifa hiyo kwa urahisi, inaweza kuwa ni taarifa gushi. Na kama ujumbe wa maandishi, video au kinganishi(link) vinaonekana kuwa ni gushi -huenda kweli vikawa ni gushi.

Herufi kubwa na muundo wa herufi haufanani basi ufahamu kuwa unafaa kuuchunguza ujumbe huo zaidi kwani ni kiashirio kuwa ujumbe huo unaweza kuwa unapotosha.

4.Hauna uhakika kuwa ni wa ukweli? Usishirikishe wengine

Usishirikishe watu wengine vitu kwa kusema “labda inaweza” unaweza kuwa ni ukweli. Unaweza kusababisha madhara kuliko kutenda wema kwa kutuma ujumbe kama huo.

Mara nying hua tunatuma vitu katika maeneo ambayo tunafahamu kuw akuna wataalamu-kama madaktari au wataalamu wa tiba . Hilo linaweza kuwa SAWA, lakini hakikisha hakikisha kwanza unaelezea wasiwasi wako kuhusu ujumbe unaoutuma . Na ufahamu -kwamba picha au maandishi unayoshirikisha yanaweza kuondlewa dhana yake baadae.

5. Tazama kila taarifa kwa umakini

Kuna ujumbe wa sauti ambao umekua ukizunguka kwenye WhatsApp. Mtu ambaye alikua anaongea katika ujumbe huo alisema kuwa anatafsiri ushauri kutoka kwa “rafiki wanaefanya nae kazi” anayefanya kazi katika hospitali . Ujumbe huo umetumwa kwa BBC na makumi ya watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

Lakini ujumbe katika sauti hiyo ni mchanganyiko wa taarifa sahihi na zisizo sahihi.

Unapotumiwa orodha ndefu ya ushauri, ni rahisi kuamini kila kitu katika ujumbe kwasababu tu unafahamu unafahamu kuwa kunawa mikono ni ukweli.

Lakini hua sio hivyo kila wakati .

Man holding garlic clovesVitunguu swaumu vinawezekana kuwa ni vizuri kwa afya lakini haviwezi kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

6. Kuwa makini na jumbe zenye hisia

Ni jambo ambalo huwa linatufanya kuwa waoga, wenye hasira, wenye wasiwasi , au kutupatia furaha ambalo husambazwa zaidi.

“Uoga ni moja ya mambo makubwa yanayosababisha kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi ,”anasema Claire Wardle wa First Draft, shirika linalosaidia waandishi wa habari kukabiliana na taarifa gushi zinazoshirikishwa kwenye mitandao .

Taarifa za miito yadharura ya kuchukua hatuahubuniwa ili kuzusha wasiwasi-kwa hivyo uwe mwangalifu.

“Watu wanataka kusaidia ndugu zai kuwa salama, kwahivyo wanapoona ujumbe unaosema ‘Mbinu za kuzuwia virusi !’ au ‘ Meza dawa hii mbadal!’ watu hutaka kufanya lolote liwezekanalo kusaidia wenzao kwa kuwatumia ujumbe huo ,” anasema.

7. Fikiria kuhusu upendeleo

Je unashirikisha kitu kwasababu inafahamu kuwa ni kweli-au tu kwasababu unaimani nao?

Carl Miller, mtafiti na mkurugenzi wa kituo cha tathmini ya mitandao ya kijamii katika taasisi ya think tank -Demos, anasema tuna uwezekano mkubwa wa kushirikisha taarifa zinazoimarisha fikra tulizonazo.

By Ally Juma.

The post Zifahamu njia saba zitakazokulinda kutosambaza taarifa za uongo kuhusu Corona appeared first on Bongo5.com.