Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limetangaza kuwa, wanajeshi 1040 wa utawala huo ghasibu wamewekwa chini ya karantini kutokana na virusi vya corona.

Televisheni ya al Alam imenukuu taarifa iliyotolewa na Aviv Kochavi, mkuu wa majeshi ya Israel akisema kuwa, utawala huo umechukua hatua hiyo ili kupunguza idadi ya wanajeshi wake waliokumbwa na virusi hatari vya corona.

Siku ya Ijumaa pia utawala wa Kizayuni ulitangaza kuwa, mwanajeshi yeyote wa utwaala huo hana ruhusa ya kuondoka kwenye ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kwamba safari za mwezi Machi za maafisa wote wa kijeshi wa Israel zimefutwa.

Mazoezi ya kijeshi ya utawala huo ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika katikati ya mwezi Machi nayo yameakhirishwa hadi wakati mwingine.

Si hayo tu, lakini pia wakazi baina ya 50 elfu hadi 80 elfu wa utawala wa Kizayuni wamewekwa kwenye karantini ya majumbani kutokana na kuenea virusi vya corona.

Advertisements

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Israel imesema, hadi hivi sasa Wazayuni wasiopungua 20 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.source https://www.muhabarishaji.com/2020/03/zaidi-ya-wanajeshi-elfu-moja-wa-israel-wawekwa-chini-ya-karantini-kwa-corona/