Watu watano wamefariki Dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo kuligonga gari dogo aina ya Toyota Noah wakati likisubiri kuvuka katika Daraja la mchepuo la Kiyegeya,Morogoro na magari yote yakatumbukia kwenye shimo ambako ujenzi unaendelea.
“Lori lililobeba shehena ya cement lilifeli breki na kugonga Noah iliyokuwa imebeba abiria eneo la Kiyegeya na kusababisha vifo vya watu wanne papohapo na mmoja wa tano amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitali”-Wilbroad Mutafungwa, RPC Morogoro.
By Ally Juma.
The post Watano wafariki kwa ajali baada ya lori na gari ndogo kugongana kwenye daraja la mchepuko Kiyegeya Morogoro – Video appeared first on Bongo5.com.