Katika kuhakikisha vita dhidi ya janga la virusi vya corona vinafanikiwa Uingereza, Waziri Mkuu, Boris Johnson amepiga marufuku mikusanyiko yote ya watu ikiwemo harusi, kuzunguka mitaani na sehemu nyingine pasipo na sababu huku katazo hilo likitoa nafasi kwa wale wanaotaka kuzika ndugu zao.
Image result for boris johnson
Uingereza, Waziri Mkuu, Boris Johnson
Bwana Boris Johnson ameyasema hayo kipindi hiki ambacho serikali ya Uingereza ikiwa na lengo la kupunguza usambaaji wa virusi vya corona.

Kwa mujibu wa The Sun, licha ya shughuli za mazishi kuruhusiwa lakini watakao takiwa kushiriki ni familia pekee na waombolezaji kukaa angalau mita mbili.

Akitoa taarifa hiyo usiku wa kuamkia leo siku ya Jumanne, Johnson amesema kuwa wamezuia mikusanyiko yote ya kijamii ambayo itaanzia watu zaidi ya wawili.

Huku wakisimamisha shughuli zote za kijamii ikiwemo Harusi, ubatizo na sherehe nyinge isipokuwa mazishi.

Watu wameshauriwa kubaki majumbani, na kutoka nje pale inapokuwa na jambo la muhimu kufanya hivyo, na kwa yoyote atakaye kiuka agizo hilo atachukuliwa hatua.

Bwana Boris Johnson amewataka wale watakaoombwa kukutana na marafiki zao, ama majirani basi waweze kukata. Na kwa wale wanaofanya mazoezi ya kukimbia, kutembea, au kuendesha baiskeli wanaruhusiwa lakini akiwa peke yake mmoja.

Wiki iliyopita baadhi ya nyumba zaibada Uingereza zilipendekeza shughuli za harusi angalao ziwe tano kwa siku ili kupunguza idadi ya watu waliotaka kufunguka ndoa. Wakati waudhuriaji awepo shahidi, bi harusi na bwana harusi.

The post Vita dhidi ya Virusi vya Corona Uingereza: Harusi, ubatizo marufuku, mazishi ruksa appeared first on Bongo5.com.