Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 11 wenye umri wa kati ya miaka 20 - 25 kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kupitia Mtandao wa Facebook kwa kutumia majina ya viongozi wa Serikali na Wasanii maarufu

Wanadaiwa kuwa walikuwa wakishirikiana na Mawakala wa kusajili laini za simu kupata laini zilizosajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzitumia kutapeli watu kwa kuwatumia jumbe fupi za simu zinazosema 'Ile pesa tuma kwenye namba hii'

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema vijana hao walifungua akaunti Facebook zenye majina ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo -