Wizara ya Afya Uganda imethibitisha kisa cha kwanza cha corona, mgonjwa ni Mwanaume Raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 36 ambae ameingia Uganda akitokea Dubai 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kuwa ifikapo saa 10:00 jioni ya Machi 22, 2020, atalihutubiwa Taifa la Uganda na kueleza ni hatua gani watachukua ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona.
 
Rais Museveni ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter

"Kutokana na uthibitisho wa kisa kimoja cha mgonjwa wa COVID-19 nchini Uganda, leo saa 10:00 jioni, nitalihutubia Taifa juu ya hatua gani zaidi za kuchukua ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Asante." ameandika Rais Museveni.