Star wa Muziki wa Country Duniani KennyRogers kutoka Marekani Amefariki Dunia akiwa na Umri wa Miaka 81, Wawakilishi wa Familia ya @_kennyrogers Wamethibiisha na Kueleza Kuwa Kenny Rodgers alipatwa na umauti akiwa Nyumbani kwake.

Kenny Rogers Alianza Ku-Hit Mwanzoni mwa Miakka ya 1970 na 1980 akishinda tuzo za Grammy 3 Na Aliwahi kuachia Track Maafuru Kama The Gambler, Luccie Pamoja na Coward of the Country.

Mwanamuziki Mkongwe na gwiji wa muziki katika miondoko ya Country, Mmarekani Kenny Rogers amefariki usiku wa kuamkia leo huko Sandy Springs, Georgia, Marekani.
Familia yake imesema Rogers aliyekuwa Mwandishi wa Nyimbo, Muigizaji, Muimbaji na ‘Producer’ amefariki kwa amani akiwa nchi ya Uangalizi wa Muuguzi huku akiwa amezungukwa na familia yake.
Rogers, alitamba kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo The Gambler, Lady, Islands in the Stream na Lucille, huku akiwa ameuza rejodi zaidi ya Milioni na kushinda tuzo 3 za Grammy.
Kama muigizaji ametokea kwenye filamu ya Six Pack mwaka 1982 na katika tamthilia kadhaa maarufu za runinga kama The Gambler franchise, Christmas in America na Coward of the County.

By Ally Juma.

The post TANZIA: Msanii mkongwe wa muziki wa country Kenny Rogers afariki dunia akiwa na miaka 81 – Video appeared first on Bongo5.com.