Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dodoma, kamati ya ujenzi wa Shule wakati walipotembelea na kujionea ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita iliyopo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ndg. Godfrey Kunambi, Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ndg. Maduka Kessy.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati) wakimsikiliza Msimamizi Mshauri wa Majengo ya Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita, Ndg. Howard Fuka tukio lililofanyika leo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Wengine ni kamati ya ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) pale viongozi wa Mkoa wa Dodoma walipokagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita iliyopo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Wa pili kulia nyuma ni Katibu.  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)