DAR: Burton Mwamba almaarufu Mwijaku, mwigizaji mtata Bongo, amesema kile alichokitabiri juu ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuhusiana na kufunga ndoa na mzazi mwenzake, Tanasha Donna, sasa yanatimia.

 

Mwijaku amefunguka hilo kufuatia sintofahamu juu ya uhusiano wa Diamond au Mondi na Tanasha huku kukiwa na tetesi kibao kuwa wameachana.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Mwijaku alisema kuwa, alishasema kuwa, wawili hao wakifunga ndoa itakuwa ni muujiza.

 

Mwijaku alisema kuwa, hakuwa anatania kwani ukweli ni kwamba, Mondi atamuacha Tanasha na kwenda kwa mwanamke mwingine na mtindo huo ataendelea nao vivyo hivyo bila hata kujali.

“Nilishasema na ninarudia tena, kinachotokea ni kwamba yale niliyosema yanatimia.

 

“Diamond kumuoa Tanasha ni muujiza, hii ni kwa sababu mbili ambazo Diamond hajamaliza kufanya. Kwanza Diamond hajamaliza kuzunguka humu nje akiwachumbia wanawake.

“Tanasha atakwenda zake na mwingine atakuja na kwenda zake. Bado ana kama miaka mitano ndipo aoe,” alisema Mwijaku.

Stori: KHADIJA BAKARI, Ijumaa