KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora ameiopongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuja kwa kampeni ya sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.

Profesa Kamuzora ameyasema hayo wakati akifungua semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera iliyoandaliwa na TCRA kutoa Elimu ya Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Katibu Tawala Profesa Kamuzora amewaomba viongozi wa dini waunge mkono serikali kupitia TCRA kueneza elimu ya Mawasiliano.

Amesema viongozi wa dini Wana wanaumini wengi hivyo ni rahisi kufikisha elimu hiyo.

"Ninaamini viongozi wa Dini mkivalia njuga basi watu wataweza kujikinga na uhalifu wakati wa wanaotumia huduma za mawasiliano"Amesema Profesa Kamuzora.

Naye Mkuu wa Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo amesema viongozi wa dini ni minutes katika kuwa daraja ya kufikisha taarifa kwa haraka na watu.


Mihayo amesema kuwa semina ya viongozi wa dini itazaa matunda kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.

Aidha amesema kuwa Kanda ya Ziwa itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania

Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.

Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.
 Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA Francis Mihayo akizungumza katika semina ya Kamati ya Amani Mkoa Kagera kuhusiana na Kampeni ya TCRA ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka.
 Sheikh wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa huo  Haruna Kichwabuta  akizungumza katika semina ya viongozi wa dini kuhusiana na Kampeni ya TCRA  Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka.
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera - Prof. Faustine  Kamuzora ,akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa  wa Kagera katika ufunguzi wa semina ya kuelimisha kamati ya Amani ya mkoa wa Kagera  jinsi ya kujikinga wanapotumia huduma za Mawasiliano ikiwa ni Muendelezo wa Kampeni ya SIRUBUNIKI “Mjanja haingizwi Chaka” inayoendelea  nchini iliyofanyika Mkoani Kagera.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joshua Mwangasa akizungumza kuhusiana na makosa ya mitandao viongoz dini  Mkoa was Kagera katika Kampeni ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka.
Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera.