KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora ameiopongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuja kwa kampeni ya sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.

Profesa Kamuzora ameyasema hayo wakati akifungua semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera iliyoandaliwa na TCRA kutoa Elimu ya Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Katibu Tawala Profesa Kamuzora amewaomba viongozi wa dini waunge mkono serikali kupitia TCRA kueneza elimu ya Mawasiliano.

Amesema viongozi wa dini Wana wanaumini wengi hivyo ni rahisi kufikisha elimu hiyo.

"Ninaamini viongozi wa Dini mkivalia njuga basi watu wataweza kujikinga na uhalifu wakati wa wanaotumia huduma za mawasiliano"Amesema Profesa Kamuzora.

Naye Mkuu wa Kanda ya Ziwa Francis Mihayo amesema viongozi wa dini ni minutes katika kuwa daraja ya kufikisha taarifa kwa haraka na watu.

Mihayo amesema kuwa semina ya viongozi wa dini itazaa matunda kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.

Aidha amesema kuwa Kanda ya Ziwa itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania

Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.

Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege Enock Walter akizungumza namna walivyopokea elimu iliyotolewa na TCRA katika Shule hiyo.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Mwandamizi Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyosimamia mawasiliano pamoja na utoaji elimu.
Afisa Masoko wa TCRA Dorice Muhimbila akimkabidhi zawadi mwalimu kutokana na kujibu swali  kwa usahihi.

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege wakisikiliza mada kutoka TCRA.