Marekani imemfungulia mashitaka Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na wasaidizi wake wakuu kadhaa kwa makosa ya ugaidi unaohusiana na ulanguzi wa dawa za kulevya. 

Aidha, imetangaza zawadi ya dola milioni 15 kwa yeyote aliye na habari zitakazopelekea kukamatwa kwake. 

Wizara ya Sheria ya Marekani imemtuhumu Maduro kwa kuliongoza genge la ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya cocaine linalofahamika kama "The Cartel of the Suns" ambalo limeingiza Marekani mamia ya tani za mihadarati kwa miongo miwili, na kupata faida ya mamia ya mamilioni ya dola.

 Wapelelezi wanasema mtandao huo wa uhalifu ulishirikiana na waasi wa FARC nchini Colombia, ambao Marekani imewaorodhesha kama "kundi la kigaidi." 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Venezuela Jorge Arreaza ameyashutumu mashitaka hayo akisema ni jaribio la mapinduzi ya Marekani. 

-DW