Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii.
BENKI ya Standard Chartered wadhamini Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwaajili ya kwenda katika uwanja wa Anfiel uliopo nchini Uingereza kwaajili ya kwenda kuangalia mchezo katika Uwanja huo.

Akizungumza  na waandishi wa habari jiji ni Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa  Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani  amesema kuwa wachezaji hao wataenda kujifunza mamo mbalimbali.

Amesema mbali na fursa mbalimbali watakazopata, Watanzania hao watashuhudia laivu moja ya mechi za Ligi Kuu ya England kati ya Liverpool na FC Bournemouth katika Uwanja wa Anfield nchini Uingereza.

"Mechi itachezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Anfield," amesema na kuongeza.

"Pia watapata fursa ya kukutana na nyota wa zamani na sasa wa klabu ya Liverpool, bahati nzuri uwepo wa Samatta (Mbwana) kwenye ligi ya kule imeifanya Tanzania kujulikana, hivyo mkatumie nafasi hii kutangaza na vivutio vya Tanzania," amesema Rughani.

Kwa Upande wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amewaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaoondoka jioni ya leo kwenda Uingereza kwa ziara ya siku tatu kwenye klabu ya Liverpool.

Msafara wa timu hiyo wenye watu tisa unaondoka nchini kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga asubuhi hii, Karia amewataka Watanzania hao kutumia vizuri fursa hiyo na kuwa mabalozi wa soka watakaporejea nchini.

"Nimeambiwa katika ziara hiyo watajifunza mambo mbalimbali kuhusu klabu ya Liverpool, uzoefu watakaoupata huko wakiutumia vema itakuwa chachu katika soka letu watakaporejea nchini.

"Naamini watajifunza miiko ya uwanja Anfield, mazingira ya klabu na nambo mbalimbali ambayo yanaihusu klabu ya Liverpool na mashabiki wake na watakaporejea itakuwa ni chachu kwao kuwapa elimu Watanzania wengine kuhusu klabu hiyo kongwe," amesema Karia.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano la Kombe la Standard Chartered lililofanyika mwaka jana pamoja na kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke(kulia) akizungumza na waandhi wa habari kuhsu wanavyoshirikiana na Benki ya Standard Chartered hasa kwenye masuala ya mpira ili kudumisha urafiki uliopo kati ya nchi mbili ambazo ni Tanzania na Uingereza wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. wa tatu kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu TFF inavyoshirikiana bega kwa bega na Benki ya Standard Chartered ili kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ili kuweza kufikia malengo yao wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani na kushoto ni Mwakilishi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, George Msonde.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars)  Ally Mayai Tembele akitoa hamasa kwa Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaosafiri leo kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani na katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege mchezaji wa timu ya Dar es Salaam Corridor wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba(kushoto) wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Majuto Omary (kushoto) kwa ajili ya kuripoti mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Liverpool na Bournemouth itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaokwenda kuishuhudia  mtanange wa Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.