Mgonjwa wa kwanza mwenye maambukizi ya virusi vya corona (covid-19) nchini Kenya amefariki katika Hospitali ya Aga Khan.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Waziri wa Afya nchini humo, Mutahi Kagwe ambaye amesema mgonjwa huyo ni mwanaume aliyekuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amelazwa Katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).
“Mwanaume huyo pia alikuwa na ugonjwa wa sukari na alikuja nchini Machi 13, 2020 kutoka Afrika Kusini akipitia Swaziland,” imesema taarifa hiyo.
Kenya hadi sasa imeripoti kesi za Corona 31 tangu kutangaza mgonjwa wa kwanza Machi 13, 2020.