Bwana Johnson amekutwa na coronavirus, baada ya kufanyiwa vipimo, imesema ofisi yake Downing Street. “Nimekuwa na dalili ndogo za coronavirus, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi ,” Bwana Johnson amesema katika video aliyoituma kweinye ukurasa wake Twitter.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa ataendelea kulingoza taifa kutoka nyumbani baada ya kupatikana na Covid-19.
Bwana Johnson atajitenga binafsi – katika makao yake ya kikazi ya Downing Street, baada ya kupimwa na kupataikana na virusi hivyo na muhusumu wa huduma za afya nchini Uingereza katika ofisi yake al maarufu No 10.

Bado ataendelea kuwa mkuu wa shughuli za kukabiliana na mzozo wa coronavirus, kulinga na taarifa iliyotolewa na ofisi yake.
“Ninafanyakazi kutoka nyumbani na nimejitenga. Hilo ndio jambo sahihi la kufanya”.
“Ninaweza kuendelea, nashukuru teknolojia kwamba ninaweza kuwasiliana na viongozi wakuu na kuongoza taifa dhidi ya virus.”, amesema.
” Kwa hiyo nashukuru sana kwa kila mtu anayefanya kile ninachokifanya, kufanya kazi kutoka nyumbani ili kuzuwia maambukizi ya virusi kutoka nyumba moja hadi nyingine”, aliongeza.
” Hivyo ndivyo tutakavyoshinda.”
Over the last 24 hours I have developed mild symptoms and tested positive for coronavirus.
I am now self-isolating, but I will continue to lead the government’s response via video-conference as we fight this virus.
Together we will beat this. #StayHomeSaveLives pic.twitter.com/9Te6aFP0Ri
— Boris Johnson #StayHomeSaveLives (@BorisJohnson) March 27, 2020

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:
Bwana Johnson alipimwa katika makazi yake baada ya kushauriwa na Mshauri Mkuu wa tiba wa England, Profesa Chris Whitty, imesema ofisi yake ya Downing Street.
Haijafahamika ikiwa Bwana Johnson ataendelea kuishi na mchumba wake Carrie Symonds, ambaye ana ujauzito wa miezi kadhaa.

Wanawake wajawazito wanashauriwa kuwa makini sana kuzingatia kuwa mbali na watu wengine katika jamii, na kupunguza utangamano wa kijamii kwa hadi wiki 12.
Kuna visa zaidi ya 11,600 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza , na watu 578 wamekwishauawa.
Hii inakuja baada ya Mwanamfalme Charles wa Wales kukutwa na virus hivyo mapema wiki hii.
Mwanamfalme Charles, mwenye umri wa miaka 71, anaonyesha dalili ndogo “lakini vinginevyo anaendelea kuwa na afya nzuri”, alisema msemaji wake.
Chanzo BBC.
By Ally Juma.
The post Hivi ndivyo Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alivyojitangaza kuwa na virusi vya corona – Video appeared first on Bongo5.com.